Connect with us

AFCON

NYOTA NIGERIA WAVUNA MILLION 76 KUIFUATA AFRIKA KUSINI.

Baada ya timu ya Taifa ya Nigeria kufuzu hatua ya nusu fainali ya fainali za mataifa ya Afrika ambazo zinaendelea nchini Ivory Coast kila mchezaji amevuna kiasi cha Million 76.

Nigeria iliiondosha klabu ya Angola kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali kwa kumshuhudia Ademola Lookman aking’ara kwenye mchezo huo.

Hata hivyo shirikisho hilo limepanga kuongeza kiasi hicho kwenye mchezo ujao wa nusu fainali dhidi ya Afrika Kusini iwapo watavuka kwenda hatua ya fainali ya AFCON 2023.

Nigeria na Afrika kusini zinatarajiwa kukutana kesho Jumatano, Feb. 7 saa mbili [20:00] usiku huku Nigeria akipewa kipaumbele zaidi cha kuibuka na ushindi kulingana na ubora wa kikosi hicho.

Kocha mkuu wa Afrika Kusini Hugo Broos amesema kuwa kwake hakuna mchezo rahisi tangu hatua ya makundi na imekuwa ikimzeesha kutokana na ugumu wa michezo hiyo.

“Kabla ya mchezo dhidi ya Cape Verde nilikuwa na umri wa Miaka 71 ila baada ya mchezo nimeongezeka umri nina Miaka 75, hizi mechi za AFCON kwangu hazijawa nyepesi mpaka sasa tangia Mechi za Makundi ni stress tupu tu”.

  • alisema kocha wa Afrika Kusini Hugo Broos.

Asilimia kubwa ya nyota wanaocheza kwenye kikosi cha Nigeria wanatoka Barani Ulaya isipokuwa golikipa wao Stanley Bobo anayekipiga Afrika Kusini kwenye klabu ya Chippa United.

Huki asilimia kubwa ya nyota wanaokipiga kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Afrika Kusini wanacheza Ligi ya ndani na wengi wanatoka klabu ya Mamelodi Sundowns.

Makala Nyingine

More in AFCON