Connect with us

Serengeti Lite Women Premier League

TFF YAILIMA JKT QUEENS FAINI MILLION 3 KISA SIMBA.

TFF imeipokonya klabu ya JKT Queens alama 5 na faini Tshs 3,000,000/= [Million tatu] baada ya kugomea mchezo dhidi ya Simba Queens uliokuwa ufanyike tarehe January 9, 2024 kwenye uwanja wa Chamazi.

Kamati ya soka la wanawake ya TFF imeamua kuipoka JKT Queens alama hizo na faini 3M kupitia kifungu cha 32-1-3 cha kanuni za ligi kuu ya wanawake 2023.

Kamati pia imewazawadia Simba Queens alama 3 na mabao 3 kwa mujibu kanuni ya 18:45 ya ligi kuu ya wanawake 2023.

Kwa mujibu wa barua ya tarehe 3 Feb 2024 yenye Kumb.Na.TFF/COMP.DEPT.24/018 iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mashindano Salum Madadi, Kamati hiyo ya soka la wanawake pia imemfungia Katibu Mkuu wa JKT Queens Duncan Malyabana kutojishughulisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi 12 kwa kuzingatia kifungu cha 32:1-5 cha kanuni za ligi kuu ya wanawake 2023.

Wakati huo huo Kamati ya soka la wanawake imeelekeza Afisa Habari wa JKT Queens MASAU KURIGA BWIRE kushitakiwa kwenye Kamati ya maadili ya TFF kwa kilichoitwa kusema taarifa za uongo kuhusu mchezo huo na kuzua taharuki kubwa.

JKT Queens walikataa kucheza mchezo huo uwanja wa Chamazi wakitaka kutumia uwanja wao wa Major General Isamuyo ulioko Mbweni jijini Dar es Salaam ambao awali ulipangwa kufanyika mchezo huo kabla ya mabadiliko ya ghafla ambayo uongozi wa JKT haukuafiki kwakuwa pia hawakupewa taarifa kwa wakati na sababu za mabadiliko zenye mashiko zaidi ya kuambiwa ni takwa la kutaka kuonyesha LIVE mchezo huo.

Katika namna ya kushangaza TFF walitaka watumie Chamazi huku wao wakisisitiza kutumia Isamuyo. Mvutano huo na tafsiri za kanuni ulipelekea mchezo huo kutofanyika kama ulivyopangwa tarehe 9 Jan 2024.

Makala Nyingine

More in Serengeti Lite Women Premier League