Timu ya Yanga imefanikiwa kuvuna alama 3 muhimu na kuwafanya wakwee kileleni mwa msimamo mbele ya Dodoma Jiji baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi kwa bao la Mudathir Yahya dakika ya 85 ya mchezo.
Yanga walianza mchezo wa kasi na dakika ya 3 tu walifanya shambulizi la hatari, krosi nzuri ya Kennedy Musonda ilitua kwenye kichwa cha Mshambuliaji Joseph Guede lakini Golikipa Mohamed Hussein alikuwa sambamba nalo.
Maxi Mpia Nzengeli alipata nafasi ndani ya kisanduku cha Dodoma Jiji akipokea pasi kutoka kwa Joyce Lomalisa dakika ya 19 ya mchezo lakini shuti lake lilimmbabatiza Nahodha Augustino Nsata.
Yanga waliendelea kulisakama goli la Dodoma Jiji lakini palikosekana umakini wa kuzitumia nafasi hizo lakini pia utasifu uhodari wa Golikipa Mohamed Hussein kuliweka lango lao salama mpaka dakika hizo.
Upande wa kulia wa Yanga, akicheza vizuri kabisa Kennedy Musonda ulionekana kuwa upande uliotumika sana kujenga Mashambulizi, Dakika ya 25 alipiga krosi nzuri lakini ilishindwa tena kutumiwa na Maxi Nzengeli na Joseph Guede.
Kukosa umakini kwa walinzi wa Dodoma Jiji almanusura kuwagharimu, Pacome Zouzoua alipata nafasi ya wazi ya kupachika bao akiwa anamtizama golikipa lakini Mohamed Hussein kwa mara nyingine tena akawaweka salama huku Kennedy Musonda akishindwa kumalizia mpira uliorejea kwake.
Dodoma Jiji waliendelea kuishi kwa hatari mpaka dakika ya 40 ya mchezo huku wakiwa wana mpira mmoja tu uliomfikia Abutwalib Mshery. Hawakuonekana kuwa hatari katika hali yoyote ile, sio kujenga mashambulizi tu lakini hata kucheza walikuwa kwenye uwezo wa chini sana wakiwaruhusu Yanga wafanye watakavyo lakini nao hawakuwa makini kutumia nyakati zao.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zikatamatika kwa timu zote kwenda kwenye vyumba vya mapumziko kwa suluhu ya 0-0
Kipindi cha pili kilirejea huku Yanga wakiendeleza walipoishia kipindi cha kwanza. Waliendelea kuwa bora sana kiwanjani huku Dodoma Jiji wakiwa bado timu ya pili. Yanga walifanya mashambulizi kadhaa dakika za mwanzo kipindi hiki cha pili lakini bado hayakuzaa matunda mpaka dakika ya 55 bado 0-0 huku Kennedy Musonda akipoteza nafasi Nyingine ya wazi akiwa karibu kabisa na goli akapaisha.
Pacome Zouzoua alipata nafasi dakika ya 61 ya mchezo lakini shuti lake hafifu lilipanguliwa na Mohamed Hussein. Wakati huo Yanga wakafanya mabadiliko kuwaingiza Clement Mzize na Mudathir Yahya nafasi za Jonas Mkude na Kennedy Musonda. Huku Dodoma Jiji wakimtambulisha mchezoni Yassin Mgaza akichukua nafasi ya Anuary Jabir ambaye hakuwa vizuri sana leo.
Yanga waliendelea kupeleka presha kwa timu ya Dodoma Jiji huku wenyewe wakiendelea kujizatiti kiulinzi. Dakika ya 76 Dodoma Jiji walifanya mabadiliko kumuingiza Paul Peter nafasi ya Gustapha Simon muda huo pia Yanga wakimtambulisha mchezoni Nickson Kibabage nafasi ya Lomalisa Mutambala.
Mohamed Hussein aliendelea kuthibitisha ubora wake katika mchezo huu akifanya uokovu mara mbili ndani ya dakika mbili akikataa kichwa cha Clement Mzize lakini kichwa kingine cha Gift Fred pia alienda nacho sambamba.
Dakika ya 85, Mudathir Yahya, Mzee wa Chamazi, aliwaainua Wananchi kwa bao la utangulizi baada ya kupokea V Pass ya Nickson Kibabage kwenye shambulizi lililoanzishwa na Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya akafanya “tap in” tu ya krosi safi kabisa kutoka kwa Kibabage. 1-0 Kwa Yanga.
Yanga walipata nafasi nyingine kupitia kwa Clement Mzize lakini Mohamed Hussein katika ubora wake hii leo akaiweka timu yake salama tena.
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...