Connect with us

AFCON

CAF: JULY TUTAPATA WACHEZAJI WENGI KULIKO JANUARY.

Shirikisho la soka Barani Afrika CAF limetangaza rasmi fainali za mataifa ya Afrika [AFCON 2025] zitakazofanyika nchini Morocco zitachezwa majira ya kiangazi kuanzia mwezi July.

Awali fainali hizo zimekuwa zikichezwa mwezi wa kwanza [January] kitu ambacho timu nyingi Barani Ulaya zimekuwa zikilalamika kuwakosa nyota wao kwasababu wapo AFCON.

Harakati za kuhakikisha michuano hii inachezwa mwezi July zilianza mara baada ya Morocco kutangazwa kuwa wenyeji wa fainali hizo za mwaka 2025.

Makamu wa pili wa Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika Ahmed Yahya raia wa Mauritania alisema kuwa wanajua kuwa kuna kombe la Dunia la klabu miezi hiyo ndio maana wakapanga ratiba baada ya fainali hizo kuisha.

“Kwa upande wetu, tunajua kuna fainali za kombe la Dunia mwaka 2025, lakini tumefanya mawasiliano kati yetu tumepata suluhisho,” Yahya alisema.

“Kitu ambacho tunaangalia ni kwa manufaa ya AFCON, kucheza kipindi cha kiangazi wachezaji wanakuwa hawapo kwenye majukumu ya klabu zao kuliko mwezi Januar,” Alisema Yahya.

Yahya aligusia pia kuhusu hali ya hewa kuwa joto nchini Morocco haitaathiri chochote kwani ipo sawa na hali ya hewa ya Ulaya.

“Morocco ina joto kama Ulaya, tumeweza kucheza European Cup kipindi cha kiangazi bila tatizo, inachezeka kipindi cha joto”, Alimaliza Yahya.

Fainali za mataifa ya Afrika zitaanza [July] mara baada ya fainali za kombe la Dunia kwa klabu kutamatika [June – July].

Kombe la Dunia kwa klabu litafanyika nchini Marekani huku Fainali za Mataifa ya Afrika zikifanyika nchini Morocco.

Makala Nyingine

More in AFCON