Connect with us

AFCON

CONGO DR NA UBINGWA WA IVORY COAST AFCON 2023.

Timu ya Taifa ya DR Congo imebeba ubingwa wa AFCON mara mbili kwenye historia yao na mara zote wamebeba baada ya kuwaondosha wenyeji wa mashindano hayo.

Leopards watashuka dimbani Jumatano hii kuikabili timu ya Taifa ya Ivory Coast ambayo ndio mwenyeji wa michuano hiyo msimu huu.

Mara ya mwisho kwa timu ya Taifa ya Ivory Coast kufika hatua ya nusu fainali ya fainali za mataifa ya Afrika [AFCON] ilikuwa mwaka 2015 na ndio walitangazwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo.

Ivory Coast wametwaa ubingwa mara mbili 1992 na 2015 huku wakimaliza katika nafasi ya pili mara mbili mwaka 2006 na 2012, Jumatano watakutana na DR Congo kwenye hatua ya nusu fainali.

Ni makala 11 kati ya 34 za AFCON ambazo zilishuhudia mwenyeji akitwaa taji la michuano hiyo, Ivory Coast haijawahi kutwaa taji hili ikiwa mwenyeji wa michuano hii, mara zote imetwaa kwenye ardhi ya ugenini licha ya kuandaa mwaka 1984.

Makala Nyingine

More in AFCON