Connect with us

AFCON

NUSU FAINALI, SOUTH AFRICA vs. NIGERIA.

Afrika Kusini inawania taji lao la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika tangu 1996, lakini wanakabiliwa na changamoto dhidi ya Nigeria ‘The Super Eagles’, katika uwanja wa Stade Bouake kwa pambano hili muhimu la nusu fainali.

TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA.

Nyota wa Napoli, Victor Osimhen alifaulu mtihani wa utimamu wa mwili na yuko tayari kucheza mchezo wa hii leo, baada ya kutosafiri na wachezaji wengine katika siku ya Jumatatu kutokana na maumivu ya tumbo.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI.

Nwabali, Bassey, Ajayi, Troost-Ekong, Aina, Iwobi, Onyeka, Sanusi, Simon, Osimhen, Lookman

TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI.

Kwa upande mwingine, Afrika Kusini haitaweza kutegemea huduma ya winga wa Mamelodi Sundowns, Thapelo Maseko, ambaye ameondolewa kwenye michuano hiyo kutokana na jeraha la misuli ya paja.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA.

Wiliams, Mudau, Modiba, Kekana, Mvala, Mokoena, Sithole, Tau, Morena, Zwane, Makgopa

TAKWIMU ZA MATAIFA HAYA MAWILI KATIKA MICHEZO ILIYOPITA.

Nigeria wameruhusu bao moja pekee hadi sasa katika michuano hiyo, huku wakiwa wamewafunga Cameroon na Angola katika hatua ya mtoano, huku Afrika Kusini ikipata ushindi kwa mikwaju ya penati dhidi ya Cape Verde katika raundi ya awali.

Hapo awali, nahodha wa Super Eagles William Troost-Ekong alifunga bao la ushindi dakika ya 89 Nigeria ilipoiondoa Bafana Bafana katika hatua ya robo fainali mwaka 2019, ambapo ilikuwa mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana.

Makala Nyingine

More in AFCON