Connect with us

Top Story

INFATINO: TUUNGANE KUKOMESHA UBAGUZI MICHEZONI.

Rais wa FIFA Gianni Infatino amerudia kauli yake ya kuchukua hatua ili kupunguza ongezeko la ubaguzi wa rangi michezoni wakati anazungumza kwenye kongamano la UEFA hapo jana.

Mwezi uliopita golikipa wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya AC Milan Mike Maignan aliondoka uwanjani wakati timu yake inacheza mchezo wa Ligi kuu nchini Italia dhidi ya Udinese kabla mechi haijaisha kutokana na kauli za kibaguzi zilizokuwa zinatolewa na mashabiki wa klabu ya Udinese.

Pia nyota wa klabu ya Coventry City inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini England Kasey Palmer alisema alikuwa mlengwa wa ubaguzi wa rangi na mashabiki baadhi wa klabu ya Sheffield Wednesday.

Matukio hayo yalimfanya Infatino ayataje kuwa machukizo makubwa, lakini pia aliongeza kwa kusema klabu zinapaswa kukumbana na adhabu ya kuondolewa alama kama mashabiki wake wataonyesha tabia ya ubaguzi wa rangi.

“Tunaishi kwenye Dunia iliyoganyika, tunasema mpira wa miguu unaiunganisha Dunia, lakini Dunia yetu imegawanyika, Dunia yetu ina fujo, wiki chache miezi iliyopita tumeshuhudia matukio mengi ya ubaguzi,” Alisema Infatino.

“Hii haikubaliki kabisa, na tunapaswa kufanya chochote tunachoweza ili kuzuia hili.”

Infatino pia aliendelea kwa kueleza kuwa mpira una vitu vyake, ambapo refa anaweza kusimamisha mchezo mara mbili na baadae kuumaliza, lakini pia vipimo vya kinidhamu na Elimu na kusema hivyo pekee havitoshi.

“Pendekezo langu juu ya haya yote ni kuwa tufanye kazi pamoja kwenye miezi mitatu ijayo kabla ya kongamano la FIFA litakalofanyika mwezi wa tano [May] Bangkok,” Infatino alisema.

“Kwenye kongamano tuje wote na maamuzi yenye nguvu, tuungane, nchi zote 211 za FIFA kupambana na huu ubaguzi wa rangi”.

“Tuumalize huu ubaguzi wa rangi, tuumalize sasa, tufanye wote kwa pamoja kwa ushirikiano.”

Makala Nyingine

More in Top Story