Connect with us

EPL

KLOPP ALIA NA MAFUA KUKABILI BURNLEY KESHO.

Kocha mkuu wa kikosi cha Liverpool Jurgen Klopp ameweka wazi kuwa kwasasa anakumbana na tatizo la kuwakosa wachezaji wengi nyota kwenye kikosi chake.

Kuelekea mchezo wake dhidi ya Burnley atawakosa Thiago (maumivu ya msuli), Dominik Szoboszlai (maumivu ya msuli), Conor Bradley (Amefiwa) and Ibrahima Konate (Anatumikia Adhabu).

Klopp amesema kesho anatarajiwa kuwakosa wachezaji wengi zaidi kutokana na ugonjwa wa mafua ulioivamia kambi hiyo hivyo atapanga kikosi kuikabili Burnley kwa kutazama nani yupo kwenye benchi.

“Tutamkosa pia Ibou, tunapambana na mafua kwenye kikosi chetu, kwahiyo tutaangalia nani atakuwepo, ni hicho tu haiko poa”.

“Lakini mwisho tutakuwa na wachezaji 11 na lazima tutacheza”.

“Mo hajarejea pia, na hilo linamaanisha kuwa tunamhitaji kila mtu”.

“Ilikuwa wiki mbili au tatu zilizopita tulikuwa tunaongea kuhusu namna ambavyo tuna machaguo mengi ya wachezaji ?”.

“Kama kuna mtu ataniuliza sasa hivi tena nitamtoa nje ya hiki chumba kiukweli. Tuliongea mara moja tu kuhusu hili na wiki moja baadae tumepata hali ya tofauti,” Alisema Jurgen Klopp.

Liverpool itashuka Dimbani kesho majira ya saa kumi na mbili [18:00] kuikabili Burnley katika mwendelezo wa Ligi kuu nchini England na kama watashinda wataendelea kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi.

Makala Nyingine

More in EPL