Connect with us

Michezo Mingine

UNAIJUA FUTSAL? TANZANIA FUTSAL KUKATA TIKETI YA AFCON LEO?

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa FUTSAL inatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Namibia kwenye mbio za kufuzu kucheza 2024 FUTSAL AFCON utakaopigwa kwenye uwanja wa ndani wa Starlight Futsal Arena uliopo Masaki, Dar es Salaam Leo hii majira ya saa 2 Usiku.

Itakumbukwa Tanzania ilipata ushindi wa mabao 5-2 ugenini, Windhoek, Namibia huku Nahodha wa Timu hiyo, mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na Mbeya City, Awadh Salum aliiongoza vema timu yake kupata ushindi huo muhimu ugenini wa ikiwa ndio mara ya kwanza Tanzania kushiriki mchujo huu wa michuano hii inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Aprili mwaka huu.

Mshindi wa Jumla anatarajiwa kukata tiketi ya kushiriki AFCON itayofanyika Aprili, 2024 huko nchini Morocco. Morocco wanakuwa wenyeji wa michuano hii kwa mara ya pili mfululizo huku wakiwa ndio Mabingwa watetezi walipotwa mwaka 2020.

Timu za Morocco, Egypt na Angola wanatarajiwa kuungana na timu 5 zitakazofuzu hatua hii ya kufuzu ili kutimiza timu 8 zitakazopepetana huko Morocco ili kupata timu 3 zitakazoenda kuwakilisha CAF kwenye FUTSAL WORLD CUP itakayofanyika huko UZBEKISTAN baadae mwaka huu wa 2024.

FUTSAL KWA KIFUPI

Futsal ni Mchezo wa Mpira wa Miguu unaochezwa kwenye Uwanja wa Ndani mara nyingi na badala ya kuwa Nyasi, unachezwa kwenye Sakafu ya Mbao(Wooden turf) kama inavyokuwaga kwenye mchezo wa Mpira wa Kikapu.

Kila Timu inaanza na Wachezaji 5 akiwemo Golikipa huku wachezaji 12 pekee ndio wanaoweza kutumika na kila timu kwenye mchezo mmoja na unachezwa kwa dakika 40 yani 20 kila kipindi pakiwa na vipindi Viwili kwa mchezo mmoja na mapumziko ya dakika 15 kila baada ya kipindi kimoja.

Hakuna offside kwenye Futsal.

Twende tukaipe nguvu timu yetu ya Taifa. HAKUNA KIINGILIO

Makala Nyingine

More in Michezo Mingine