Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja vitatu tofauti nchini.
Mchezo mkubwa unaotarajiwa kutazamwa na wengi ni kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya wajelajela klabu ya Tanzania Prison, kuelekea mchezo huo hizi ndio takwimu za timu zote mbili.
16:00 Tanzania Prison vs Yanga.
Uwanja: CCM Sokoine, Mbeya.
- Timu hizi zimekutana mara 24 hivi karibuni, Yanga ikishinda mara 16, Tanzania Prison haijapata ushindi na sare nane [8].
- Yanga imeifunga Prison magoli 40 kwenye michezo 24 na Prison imefunga magoli 13.
- Yanga imeshinda michezo saba [7], imetoa sare michezo mitano [5] ikiwa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons kati ya michezo 12.
- Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa kinara na alama 37 katika michezo 14 ya Ligi iliyocheza, huku Tanzania Prison wakicheza michezo 14 na alama 17 wakiwa nafasi ya tisa [9].
- Klabu ya Yanga msimu huu ikiwa ugenini imecheza michezo sita [6], imeshinda michezo minne [4], imepoteza mchezo mmoja [1] na imetoa sare mchezo mmoja [1], ikivuna alama 13, wameruhusu magoli matatu [3] na kufunga 11.
- Tanzania Prison wakiwa nyumbani msimu huu, wamecheza michezo saba [7], wameshinda michezo mitatu [3], wametoa sare michezo miwili [2], na kupoteza michezo miwili [2], wameruhusu magoli saba [7] na wamefunga magoli saba [7].
Leo pia kutakuwa na maadhimisho ya miaka 89 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Yanga na yatafanyika Jijini Mbeya ambapo mchezo wa leo umetanguliwa na shughuli za kijamii ambazo zilifanywa na mashabiki hapo jana.
Michezo mingine ya Ligi hii leo,
14:00 Tabora United vs Namungo.
19:00 Dodoma Jiji vs Mashujaa.