Connect with us

Top Story

MESSI MILANGO IPO WAZI KUSHIRIKI OLYMPIC 2024.

Nyota wa klabu ya Inter Miami na timu ya Taifa ya Argentina, Leonel Messi anatajwa kujumuika na kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina U23 kwenye fainali za Olympic ambazo zitafanyika Paris Nchini Ufaransa.

Argentina imefuzu kwenye michuano ya Olympic 2024 baada ya kuwaondoa mabingwa wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Brazil kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kishiriki michuano hiyo.

Mara ya mwisho kwa timu ya wanaume ya Argentina kushinda michuano hiyo ilikuwa mwaka 2008 iliyofanyika nchini Beijing na Messi alikuwa sehemu ya kikosi hicho.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina U23 Thiago Almada amesema anatumaini Messi atajiunga na kikosi hicho kwenye majira ya joto mwaka huu na atampatia kitambaa cha unahodha.

“Natumaini Messi atakuwepo kwenye michezo ya Olympic,na itakuwa ndoto”

“Kama Messi ataungana na sisi basi nitampa kitambaa cha unahodha”, Alisema Thiago.

Kocha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina U23 ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa zamani Javier Mascherano amemfungulia milango nyota huyo ili ajiunge na kikosi hicho kwaajili ya michezo ya Olympic.

“Kila mtu anafahamu uhusiano wangu na Leo [Messi], na urafiki tulionao”.

“Mchezaji kama yeye milango ipo wazi kwenda na sisi [Olympic], sasa itabakia kwake na uamzi wake”, alisema Mascherano.

Kwenye michuano ya Olympic licha ya kujumuisha wachezaji wenye umri mdogo lakini pia yanatoa nafasi chache kwa wachezaji wenye umri mkubwa kujiunga na vikosi vya timu za Taifa zilizofuzu ili kuongeza chachu ya ushindani kwa vijana.

Makala Nyingine

More in Top Story