Nyota wa zamani wa klabu ya Yanga Fiston Kalala Mayele jana alitoka mtandaoni na kudai kuwa viongozi wa klabu ya Yanga na mashabiki wake wanamchukia licha ya kuwa sio Mtanzania.
Kalala alienda mbali zaidi na kudai kuwa anatumiwa majini na viongozi hao ili asifanye vizuri hupo alipo [Pyramids] akiamini kuwa ni kweli ametumia na ndio maana hafanyi vyema kwasasa kama alivyokuwa anafanya Yanga.
“Chuki ni ya nini, mimi sio Mtanzania mbona, nilikosea kucheza timu za Tanzania nini ?”, aliandika Fiston Mayele.
Baada ya taarifa hiyo kutoka mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga Mrisho Khalfan Ngassa nae akatoa maoni yake kwa kusema kama mambo ya kutupiana majini yapo basi yeye au Feisal Salum wangekuwa wamechanganyikiwa.
Ikumbukwe Feisal aliondoka Yanga baada ya purukushani nyingi kwenda Azam na Mrisho Ngassa aliwahi pia kuhamia Azam akitokea Yanga.
” Kuna kipindi nilihamia timu nyingine kutoka yanga, nikakuta kule mashabiki wachache nishazoea shangwe kufunga kukawa shida, nikasema ndio nimeisha au lakini sikuwaza majini.”
“Kuna wachezaji wakitoka Simba, Yanga au Azam kufunga ni ngumu wanaenda timu ina mashabiki 30 mpinzani haogopi chochote, uwezo wako ndio unatakiwa uuonyeshe”.
Umeuzwa, watu wamepiga pesa, wamefurahi, baadae unalalamika umetupiwa jini, kama ni hivyo basi Feisal Salum [Fei Toto] angekuwa chizi, majini ya kusafiri na majini ya hapa hapa yanamuona”.
“Timu ni kubwa kuliko mtu yoyote, hii ni stori fupi wachezaji Kuna maisha baada ya mpira, tuishi vizuri na shule tulizo pita, kesho tutasomesha watoto wetu Kwa Ada ndogo”, Aliandika Mrisho Ngassa.
Malalamiko hayo ya Mayele yalikuja baada ya timu ya Taifa ya Congo DR kupoteza mchezo wao wa mshindi wa tatu dhidi ya Afrika Kusini ambao pia alicheza na kukosa nafasi kadhaa za wazi.