Connect with us

NBC Premier League

TANZANIA PRISON KUREJESHA HESHIMA BAADA YA KIPIGO.

Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga (2-1) kwenye uwanja wa CCM Sokoine, Jijini Mbeya inatarajiwa kushuka dimbani tena kesho kuikabili klabu ya Singinda Fountain Gate.

Kuelekea mchezo huo kocha wa kikosi cha Tanzania Prison Hamad Ally amesema makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga wameyafanyia kazi na hayatajirudia tena.

“Tunauhitaji wa matokeo kwa siku ya kesho, tunamuheshimu mpinzani wetu, ni timu nzuri, ipo na wachezaji wazuri na staff nzuri, tunaamini kabisa utakuwa ni mchezo mgumu”.

“Tulifungwa goli mbili na Yanga ni kwasababu ya makosa madogo sana, tumeangalia video kwenye mechi dhidi ya Yanga na tumefanya marekebisho”, alisema Hamad Ally kocha mkuu wa Prison.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa klabu ya Singida Fountain Gate ambayo pia imetoka kupoteza mbele ya Kagera Sugar Nizar Khalfan amesema Ligi ni ngumu na kila timu imejipanga.

“Ligi ni ngumu kila timu imejipanga, timu zilizopo mkiani zinataka kujikwamua, lakini sisi bado tuna uwezo wa kupambana na tunajua hata Tanzania Prison watatupa changamoto”.

“Naamini kesho tutapata ushindi kwa sababu hatutakubali kupoteza mechi mbili mfululizo”, Nizar Khalfan.

Mchezo huo wa Tanzania Prison na Singida Fountain Gate utachezwa saa kumi jioni kwenye uwanja wa CCM Sokoine mkoani Mbeya.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League