Klabu ya Simba leo itashuka dimbani ugenini kwenye mwendelezo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara kuikabili klabu ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni Jijini Dar Es Salaam.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Simba kukutana na JKT Tanzania kwenye uwanja huu wa Jenerali Isamuhyo kwenye mchezo utakaopigwa saa kumi [10:00] jioni.
Kuelekea mchezo huu hizi hapa ni takwimu za timu hizi mbili kuanzia zilipoanza kukutana.
- Kwa kipindi cha hivi karibuni klabu ya Simba na JKT Tanzania zimekutana mara sita [6], Simba imeshinda mara tano [5], JKT Tanzania ikishinda mara moja [1] pekee.
- Klabu ya Simba imeifunga JKT Tanzania magoli 13 na JKT Tanzania imeifunga Simba magoli mawili [2] tangu msimu wa 2018/19.
- JKT Tanzania haijawahi kupata ushindi mbele ya Simba ikiwa mwenyeji wa mchezo, imecheza michezo mitatu [3] na imepoteza kwa magoli 3+.
- Mara ya mwisho JKT Tanzania kushindi ilikuwa ugenini msimu wa 2019/2020, ilishinda kwa goli 1-0.
Takwimu za msimu huu wa 2023/24 kwa timu zote mbili yaani Simba na JKT Tanzania.
- Simba ipo nafasi ya pili [2] ya msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara kwasasa, huku JKT Tanzania ikiwa nafasi ya 12 na timu zote zimecheza michezo 14.
- Simba hadi hivi sasa imekusanya alama 33, imefunga magoli 30 na kuruhusu magoli 14.
- Katika michezo yao 14 waliyocheza Simba imepoteza mchezo mmoja [1], sare tatu [3] na imeshinda michezo 10.
- JKT Tanzania imekusanya alama 16, imefunga magoli 12 na imeruhusu magoli 18.
- Katika michezo yao 14 waliyocheza JKT Tanzania wameshinda michezo minne [4], sare michezo minne [4] na imepoteza michezo sita [6].
Simba ina wastani wa kuruhusu goli moja [1] kwa kila mchezo na ina wastani wa kufunga magoli mawili [2] huku JKT Tanzania ikiwa na wastani wa kuruhusu goli moja [1] kila mchezo na wastani wa kufunga goli 0.85.