Connect with us

Boxing

TPBRC: MWAKINYO HAWEZI KUPIGANA NA KIDUKU.

Kwa siku za hivi karibuni zimekuwa zikitoka taarifa za kuhitaji kupigana kwa mabondia wakubwa nchini Tanzania Hassan Mwakinyo na Twaha Kiduku jambo ambalo limezua hisia tofauti kwa wapenzi wa ngumi nchini.

Taarifa zimekuwa zikienea kuwa mapromota wa pambano hili wamejitokeza na kuweka pesa nyingi kwaajili ya kulifanikisha pambano lakini kila upande wa mabondia umekuwa hauridhiki na kiasi hicho.

Katibu wa bodi ya ngumi za kulipwa nchini TPBRC George Silas ameweka wazi kuwa mabondia hao hawawezi kupigana kwasasa kutokana na uzito wao kuwa tofauti lakini kama wakiwa sawa wanaweza kupigana.

“Twaha Kiduku na Mwakinyo ni uzito tofauti, Twaha Kiduku anachezea Super Middle kilo 76, Mwakinyo anachezea Super Welter kilo 69, mabondia wanapigana wakiwa na uzito sawa”.

“Kama Mwakinyo ana kilo 69, anataka kupigana na Twaha anatakiwa apande, au Twaha ashuke, sisi kama kamisheni hatuwezi kuwaruhusu kwasababu uzito ni tofauti”.

“Ni pambano zuri, tuwaombe mapromota wawekeze kwenye pambano hili” George Silas Katibu wa TPBRC.

Mwakinyo na kiduku wamekuwa alama ya mchezo wa masumbwi nchini kutokana na mafanikio ambayo wameyapata kwa miaka ya hivi karibuni kwenye masumbwi.

Hata hivyo nyota hawa waliwahi kufanya kazi pamoja na sasa kila mmoja amekuwa akimrushia kijembe mwenzake na hadi hivi sasa hakuna taarifa zozote juu ya kufanyika kwa pambano hili.

Makala Nyingine

More in Boxing