Connect with us

Makala Nyingine

TAKWIMU ZA KMC DHIDI YA YANGA KUELEKEA MECHI YA LEO.

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa kati ya klabu ya Kinondoni MC na Yanga zote za Dar Es Salaam.

Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Jamhuri, mkoani Morogoro majira ya saa kumi [10:00] jioni.

  • Kuelekea mchezo huu takwimu zinaibeba zaidi Yanga kwani katika michezo 11 ya hivi karibuni Yanga imeshinda michezo nane [8] na imetoa sare mara mbili [2] huku KMC ikipata ushindi mara moja [1].
  • Yanga imeifunga KMC magoli 18 huku ni mchezo mmoja [1] pekee uliomalizika bila Yanga kupata goli lolote na michezo yote kumi iliyosalia Yanga imefunga walau goli moja [1].
  • KMC imeifunga Yanga magoli matano [5] na msimu huu kwenye mchezo wa kwanza ilikubali kichapo cha goli tano [5].
  • Yanga inaongoza kundi ikiwa imekusanya alama 40 katika michezo 15 ambayo imecheza msimu huu na ndio mabingwa watetezi wa Ligi hii.
  • KMC ipo nafasi ya tano [5] ya msimamo wa Ligi ikiwa imecheza michezo 15 imekusanya alama 22.
  • Msimu huu Yanga imefunga magoli 36 na kuruhusu magoli 8 na KMC imefunga magoli 15 na kufungwa magoli 21.
  • Yanga imeshinda michezo 13, imetoa sare mchezo mmoja [1] na kupoteza mchezo mmoja [1] hadi hivi sasa.
  • KMC wameshinda michezo mitano [5], Sare michezo saba [7] na kupoteza michezo mitatu [3].

Yanga inanafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo kutokana na urejeo wa golikipa wake Djigui Diarra na kiungo wake Aziz Ki waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya za Taifa kwenye mashindano ya AFCON.

Timu yoyote itakayoshinda hapa itakuwa imepata ushindi wake wa kwanza kwenye mzunguko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine