Connect with us

CAF Champions League

SIMBA KUIFUATA ASEC IVORY COAST ALFAJIRI.

Klabu ya Simba inatarajiwa kuanza safari Jumatano Alfajiri kuelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika.

Simba itashuka dimbani kuikabili Asec Mimosas siku ya ijumaa usiku majira ya saa nne [22:00] kwa saa za Afrika mashariki,

Simba itawakosa nyota wake kadhaa akiwemo mlinda lango wao Ayoub Lakred, John Bocco, Aubin Kramo, Ladack Chasambi, Edwin Balua na wengine.

Kuelekea safari hiyo Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally ametoa sababu za nyota hao kukosekana kwenye safari hiyo.

“Saa tisa Alfajiri safari ya kuelekea Ivory Coast inaanza, tutaondoka na wachezaji 23, benchi la ufundi, pamoja na maafisa kutoka Simba [Bodi ya wakurugenzi], jumla ya msafara ya watu wasiopungu 40 watakuwa safarini”.

“Baadhi ya wachezaji watakosekana kwa sababu mbalimbali, Ayoub Lakred atakosekana kutokana na kadi tatu za njano, John Raphael Bocco na Willy Onana ambao ni majeraha, wachezaji wengine watakosekana kwasababu hawapo kwenye mpango wa mwalimu”, amesema Ahmed Ally.

Kikosi cha Simba ambacho kitasafiri kuelekea nchini Ivory Coast kitajumuisha wachezaji 22.

MAGOLIKIPA

  1. Aish Manula
  2. Ally Salim
  3. Hussein Abel

WALINZI

  1. Shomari Kapombe
  2. Israel Mwenda
  3. David Kameta Duchu
  4. Mohamed Hussein
  5. Henock Inonga
  6. Che Fondog Malone
  7. Kennedy Juma
  8. Hussein Kazi

VIUNGO

  1. Babacar Sarr
  2. Sadio Kanoute
  3. Fabrice Ngoma
  4. Mzamiru Yassin
  5. Abdallah Hamis
  6. Said Ntibanzokiza
  7. Kibu Dennis
  8. Luis Miquissone
  9. Clatous Chama

WASHAMBULIAJI

  1. Pa Omar Jobe
  2. Fredy Michael

Makala Nyingine

More in CAF Champions League