Oscar Mirambo mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la ufundi nchini Tanzania ameeleza namna ambavyo nchini imefanikiwa baada ya kushiriki michuano mikubwa ya AFCON U17 kwa makala tatu, ikiwemo kuzalisha wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi.
“Tumecheza makala tatu za AFCON U17 tumecheza [2017, 2019 na 2021], na tumezalisha wachezaji 13 wanaocheza nje ya Tanzania”.
“Ligi kuu na Champioship zimetawaliwa na hiki kizazi, kama tutacheza makala 10 za AFCON maana yake tutazalisha wachezaji 130 watakaocheza nje”, alisema Oscar.
Kwa upande mwingine kila timu ya Taifa inapoitwa maneno yamekuwa mengi kuhusu kuachwa na kuitwa kwa baadhi ya wachezaji, huku Oscar Mirambo akitolea ufafanuzi kuwa uamuzi wa kuwaita wachezaji upo mikononi mwa mwalimu.
Wadau wa michezo nchini wamekuwa wakihoji nafasi ya Mkurugenzi wa michezo kwenye kuita timu ya Taifa lakini yeye amejibu kuwa ofisi yake haiwezi kuingilia maamuzi ya mwalimu.
“Siwezi kuamua kuita mchezaji kwenye timu ya Taifa, mimi naweza kushauri na kuweka mapendekezo ya kwangu, uamuzi wa mwisho ni wa mwalimu”.
“Maamuzi lazima yabaki kwa mwalimu na hiyo ndio professionalism, Kama wewe ni kocha mkuu halafu maamuzi yanafanywa na mtu mwingine, nani sasa ni kocha ?”, aliongeza Oscar Mirambo.
Hata hivyo Oscar Mirambo ametanabaisha kuwa hadi hivi sasa mezani kwake kuna takribani majina 106 ya wachezaji wenye unasaba na Tanzania wanaokipiga nje ya nchi na kila kocha akija anakabidhiwa faili la nyota hao ili awafuatie maendeleo yao.
“Tunawachezaji takribani 106 wanaocheza nje ya nchi ambao ni watanzania”, alimaliza Oscar Mirambo, Mkurugenzi wa ufundi TFF.