Connect with us

CAF Champions League

KOCHA ASEC MIMOSAS AKIRI UGUMU KUCHEZA NA SIMBA LEO.

Kocha mkuu wa klabu ya Asec Mimosas Julien Chevalier amesema kuwa wamekutana na wakati mgumu baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wao Karamoko Sankara.

Sankara aliuzwa na klabu ya Asec Mimosas kuelekea klabu ya Wolfsberger AC ya nchini Australia kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi January.

“Wiki mbili zilizopita nimekutana na changamoto ya kujenga safu mpya ya ushambuliaji baada ya kuondoka Sankara Karamoko, ambaye ameuzwa kwenye dirisha la usajili la mwezi January kwenda Wolfsberger AC ya Ligi kuu nchini Australia”.

“Wapinzani wetu wamefanya maingizo mapya na wamefanya mabadiliko makubwa tangu tukutane mara ya mwisho, kwahiyo tunajiamini kwasababu tunacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani”, Chevalier, Kocha wa Asec Mimosas.

Hata hivyo klabu ya Asec Mimosas ilikuwa tayari imeanza maisha bila ya uwepo wa nyota huyo baada ya kuanzia benchi kwenye baadhi ya michezo ya klabu hiyo.

Klabu ya Simba pia imefanya maingizo ya nyota wapya kwenye kikosi chao kwenye dirisha dogo la usajili kwa kuwaingiza Pa Omar Jobe, Fredy Koublan na Babacar Sarr huku ikiwaondosha washambuliaji wake waliokuwa na wastani bora wa ufungaji wa magoli.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League