Connect with us

Top Story

NYOTA QPR AHUKUMIWA JELA BAADA YA KUMVUNGA FUVU DEREVA.

Klabu ya QPR imetoa waraka kuhusu kesi iliyokuwa ikimkabili nyota wake raia wa Morocco Ilias Chair ambaye amehukumiwa jela mwaka mmoja na ongezeko la miezi 12 na makahama ya Antwerp ya nchini Ubelgiji ambapo amekulia.

Hukumu hiyo pia inamhusu kaka yake Chair anayeitwa Jaber, tukio hilo limetokea baada ya ugomvi kati yao na dereva wa roli anayejulikana kwa jina la Niels T.

Ugomvi huo ulisababisha majeraha makubwa ikiwemo dereva huyo kuumia kwenye kichwa baada ya kupigwa jiwe kichwani lililorushwa na nyota huyo wa QPR.

Mahakama pia imemuamuru Chair kulipa kiasi cga £ 13,400 [TZS Million 43.4], kama fidia kwa dereva aliyepigwa na jiwe kichwani.

Upelelezi wa kisheria bado haujafika mwisho, kwa maana hiyo klabu haitatoa neno lolote kwenye hatua hii.

Taarifa ya QPR inasema

Licha ya ubora alionao Chair ndani ya QPR msimu huu akicheza michezo 31, amefunga magoli manne, na pasi za usaidizi tano kwenye Ligi daraja la kwanza lakini kwa hali mbaya klabu inahangaika kutokushuka daraja.

Makala Nyingine

More in Top Story