Klabu ya Simba inatarajiwa kushuka dimbani jumatano hii kuikabili klabu ya TRA kwenye mwendelezo wa kombe la shirikisho [ASFC] nchini Tanzania, mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi Jijini Dar Es Salaam.
Simba itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa March 2.
Kuelekea mchezo wa Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy, Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameweka wazi kuwa klabu yake inahitaji kufuzu hatua ya robo fainali ili kuungana na wakubwa wenzao wanne huku Yanga akiiondoa kwenye kundi la timu kubwa Barani Afrika.
Tukifanikiwa kufuzu robo fainali tutakuwa tumeungana na timu zingine kubwa barani Afrika ambazo zimewahi kuingia robo fainali mara nne mfululizo. Hapa nazungumzia Al Ahly, Mamelodi, Wydad na TP Mazembe na sisi tunakwenda kuwa timu ya tano.
Afisa Habari wa Simba SC Ahmed Ally.
Simba inahitaji ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy ili ijihakikishie nafasi ya kufuzu hatua ya Robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika, kama itafanikiwa kufuzu itakuwa mara ya nne kwa Simba kwa miaka ya hivi karibuni kufuzu hatua hii.
AHMED ALLY – AFISA HABARI SIMBA.
Inonga mgeni rasmi mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy lakini sio lazima kujiweka kama yeye, Tunampa heshima Inonga kwa makubwa aliyofanya AFCON lakini niseme haina haja ya kuwa kama INONGA tumpe heshima lakini haina haja kuwa kama Yeye.
Wakati Mo Dewji anatengeneza ramani za kutawala soka la Africa klabu zote zilikuwa zimelala.
Sisi Simba na Mo Dewj tumetengeneza ramani ya kuifanya Yanga kufuzu robo finali kwa mara ya kwanza.
Robo fainali ya Bwana wale anaepaswa kupongezwa ni Mo Dewj kwa sababu aliwaamsha wenzie kulitawala soka la Africa.
Sisi sio waoga wa mechi za kimataifa, sisi hatuogopi kwasababu sio wadhaifu maana mtu muoga siku zote ni dhaifu, sisi ndio tunaogopwa Afrika nzima kwenye mashindano ya CAF Champions League, ila kwa upande wa tahadhari tumechukua tahadhari kubwa kuliko mechi zote tulizocheza.