Connect with us

Simba

MECHI YA SIMBA NA JWANENG KUPIGWA SAA MOJA JIONI.

Klabu ya Simba itashuka dimbani Jumamosi, March 02 kuikabili klabu ya Jwaneng Galaxy, mchezo ambao utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam. Huu utakuwa mchezo wa nne kwa klabu hizi mbili kukutana huku kila timu ikishinda mara moja na sare mchezo mmoja.

Afisa habari wa klabu ya Simba ametanabaisha kuwa wao waliomba mchezo huo uchezwe saa kumi [16:00] jioni lakini kwasababu shirikisho la soka Barani Afrika [CAF] walitaka michezo yote ichezwe muda sawa wakaelekeza mchezo huo upigwe saa moja [19:00] usiku.

Simba inasaka ushindi wa aina yoyote ile ili iweze kufuzu hatua ya robo fainali na ikitokea matokeo tofauti basi inaweza kuwapa ugumu zaidi Simba. Simba haijawahi kupata ushindi mbele ya Jwaneng Galaxy kwenye uwanja wa Taifa na mara ya mwisho walipoteza.

AHMED ALLY – AFISA HABARI SIMBA SC

Mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy itachezwa Jumamosi Machi 2, 2024 saa 1:00 usiku. Licha ya mapendekezo yetu kucheza mechi saa 10:00 jioni lakini CAF wameamua iwe saa 1:00 usiku ili michezo yote iwe muda mmoja.

Kikosi kimerejea nchini na leo jioni tutaanza rasmi mazoezi kujiandaa na mchezo Jwaneng Galaxy na mchezo wa ASFC dhidi TRA ambao tutacheza Jumatano kwenye uwanja wa Azam Complex.

Waamuzi wa mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy wataanza kuwasili nchini kuanzia tarehe 29 mwezi huu na wote wanatokea nchini Ghana.

Mpaka sasa hatujapata taarifa rasmi Jwaneng Galaxy lini watawasili nchini lakini watu wao wa maandalizi ya awali wameshawasili nchini.

Ushindi wa aina yoyote ambao tutapata Jumamosi sisi tutafuzu bila kujali Wydad kapata ushindi wa aina gani. Sisi na Wydad tukishinda tutakuwa na alama tisa na kanuni ya kwanza ya CAF inaangalia Head to Head, mechi ya kwanza walitufunga goli 1-0 na sisi tukawafunga 2-0.

Tangu tumeanza kampeni ya kimataifa hatujawahi kuishia hatua ya makundi, hatujawahi kufungwa mechi ya mwisho ya maamuzi ya kwenda robo fainali. Simba Sports Club inapofika hatua kama hii anakuwa mnyama mwingine wa ajabu.

Hatujawahi na hatutakuja kuishia hatua ya makundi, achana na watu wanaochanganyikiwa na ushindi wa goli 4, Mnyama tumeshamfanya mtu goli 7 na tukaenda robo fainali.i

Ahmed Ally, Akizungumza na waandishi wa habari leo.

Makala Nyingine

More in Simba