Connect with us

Top Story

SERIKALI CAMEROON KULICHUNGUZA SHIRIKISHO LA SOKA.

Taarifa kutoka nchini Cameroon zinasema kuwa Rais wa nchi ya Cameroon Paul Biya ameamua kuingilia kati uteuzi wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Cameroon.

Taarifa zinasema uteuzi wa kocha mpya hautamhusisha Rais wa sasa wa shirikisho la soka nchini humo Samuel Eto’o hasa baada ya kufeli kwenye uteuzi wa kocha wa sasa.

Samuel Eto’o alipewa uhuru wa maamuzi kwenye uendeshaji wa shirikisho la soka nchini Cameroon na vitu vingine lakini yamekuwa majanga ndio maana serikali ikaingilia kati kuweka mambo sawa.

Ofisi wa Waziri mkuu imepokea maagizo ya kuunda kamati kutoka kwa Rais ili ifanye uchunguzi wa kujua nini tatizo na namna bora ya kutatua changamoto hizo.

Kamati hiyo imeundwa na watu kutoka ofisi ya Waziri mkuu, Ofisi ya Rais, na wizara ya michezo lakini Rais wa shirikisho hilo Samuel Eto’o si sehemu ya kamati hiyo.

Makala Nyingine

More in Top Story