Connect with us

Makala Nyingine

DIENG: YANGA INAWEZA KUCHEZA FAINALI CAF CL.

Kiungo wa Al-Ahly ameitabiria makubwa klabu ya Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu.

“(Al-Ahly) Tulikuwa tunaangalia mechi yao iliyopita (Yanga SC 4 – 0 Belouizdad), kila mmoja alishangaa kwa kiwango ambacho Yanga walikionesha kwenye Mchezo huo”

“Ukikumbuka kiwango chao tulipokutana nao (Yanga 1 – 1 Al-Ahly) + hiki walichofanya kwa CR Belouizdad utaona hii timu ina uwezo mkubwa kwa sasa Africa, sitashangaa kuona wanacheza nusu fainali au hata fainali (CAF-CL) kama wakikutana na timu ya Kawaida kwenye hatua ya robo fainali”

“Kitu ambacho kimewapa nguvu ni kuwa na wachezaji bora sana ambao wamekuwa wakiamua matukio magumu uwanjani mfano Djigui Diarra. Diarra ni mchezaji muhimu sana kwenye timu yetu ya taifa ya Mali vivyohivyo kwa Yanga”

“Nimekuwa nikiifatilia Yanga muda mrefu kupitia kwa Djigui Diarra ni timu nzuri inayocheza mpira mzuri wakuvutia”

-Aliou Dieng
Kiungo wa Al-Ahly

Aliou Dieng atashuka dimbani na klabu yake ya Al Ahly kesho Ijumaa majira ya saa moja [19:00] jioni dhidi ya Yanga katika mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi.

Mshindi wa mchezo huo wa kesho atapata nafasi ya kuongoza kundi lake ambapo kwasasa Al Ahly [9] inaongoza kwa tofauti ya alama moja na Yanga [8].

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine