Connect with us

CAF Champions League

SIMBA KUANDIKA HISTORIA MPYA LEO.

Klabu ya Simba ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika utakaopigwa saa moja [19:00] jioni Jijini Dar Es Salaam leo March 02, 2024.

Klabu ya Simba itaingia kwenye mchezo huu ikisaka ushindi ili ifikishe alama tisa [9] na iweze kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika ikiungana na Asec Mimosas kwenye kundi B.

Hii itaifanya Wydad AC iondoshwe kwenye michuano hii hata kama ikishinda na kuwa na alama sawa na Simba, kwani kigezo kinachotazamwa ni idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga timu hizo mbili zilipokutana ambapo Simba ana faida ya goli moja baada ya mchezo wa kwanza kushinda 2-0 nyumbani na kupoteza 0-1 ugenini dhidi ya Wydad.

Jwaneng Galaxy pia ina nafasi ya kufuzu kama ikishinda mchezo wake dhidi ya Simba hii leo kwani itafikisha alama saba [7] lakini itakuwa inaiombea matokeo chanya Asec Mimosas kwenye mchezo wao dhidi ya Wydad AC.

Jwaneng Galaxy iliwahi kuitoa Simba kwenye mzunguko wa pili wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika kwenye dimba hilo hilo la Benjamini Mkapa, Simba ilishinda goli 2-0 nchini Botswana na kupoteza 3-1 kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Simba ikifuzu robo fainali leo itakuwa mara ya nne kufuzu hatua hii ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika na itakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kupeleka timu mbili hatua ya robo fainali.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League