Connect with us

Makala Nyingine

DUBE AOMBA KUTIMKA AZAM

Klabu ya soka ya Azam FC imethibitisha kupitia kwa Afisa Habari wake Thabith Zakaria “ZakaZaKazi” kuwa imepokea barua ya maombi ya kuvunja mkataba wake kutoka kwa Mchezaji wao Prince Mpumelelo Dube.

Katika Maelezo yake, Zaka alisema

Tunathibitisha kupokea barua ya kuomba kuvunja mkataba kutoka kwa Prince Dube ambaye amekuwa mchezaji wetu tangu mwaka 2020 na hivi karibuni alisaini mkataba ambao unamalizika mwaka 2026.

Aidha Zaka alisema kuwa wao hawana pingamizi ila taratibu za kawaida zifuatwe.

Sisi hatuna pingamizi juu ya ombi lake na Klabu inamruhusu kuondoka ila kwa mahitaji ya mkataba kwamba lazima Mkataba utekelezwe kama unavyotakiwa kwani mpaka sasa bado ana mkataba wa miaka miwili na nusu (2.5) na hivyo kunakuwa na gharama zake na mambo mengi yataendelea.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Timu imempa machaguo ya namna ya kuachana na klabu.

Tumemwambia kuwa chaguo la kwanza ni kama kuna timu ambayo imevutiwa na huduma yake na inataka kumnunua ije ikae mezani na Azam na gharama yake ni Dola 300,000(Takribani Milioni 750 za Kitanzania) au chaguo la pili asalie kwenye klabu mpaka mkataba utakapomalizika ili aweze kuondoka.

Bado haijafahamika wazi sababu za Prince Dube kuomba kuondoka ila anahusishwa na vilabu vingine vikubwa hapa nchini huku Azam FC ikisisitiza kuwa iko tayari kumuachia wakati wowote matakwa ya kimkataba yakikamilika.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine