Connect with us

Makala Nyingine

KASUNDA AMTAJA NYOTA HATARI NCHINI ALIYESTAAFU MDOGO.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Azam, Mbeya kwanza na sasa klabu ya Dodoma Jiji, Paul Peter Kasunda amemtaja Mbwana Samatta kuwa mchezaji wake bora wa muda wote kutoka Tanzania.

Nafikiri Mbwana Ally Samatta ndiye mchezaji bora wa muda wote kutoka Tanzania, hii ni kutokana na mafanikio aliyoyapata na namna alivyowavutia vijana wengi kupenda soka na kuamini katika vipaji vyao.

Paul Peter mshambuliji wa Dodoma Jiji.

Paul Peter amepata malezi yake ya soka kwenye Academy ya Azam FC iliyopo Dar Es Salaam na akacheza klabu kadhaa kwa mkopo ikiwemo Mbeya kwanza na baadae kutimkia Dodoma Jiji.

Kasunda pia amemtaja Kelvin Chale kuwa miongoni mwa wachezaji mahili sana ambao aliwahi kuwashuhudia wakicheza mpira hapa Tanzania lakini kwasasa amestaafu soka akiwa na umri mdogo na anaishi Uturuki kwasasa.

Kelvin Chale aliwahi kucheza klabu ya Simba ya vijana na alitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa kuchungwa zaidi kwa siku za usoni lakini masomo yakawa kipaombele zaidi kwake na kuachana na mpira.

Kuna jamaa anaitwa Kelvin Chale aliwahi kucheza klabu ya Simba ya vijana, kwa hapa Tanzania sijawahi kuona kama yeye jamaa anajua sana.

Chale kwasasa amestaafu amechagua kusoma zaidi akaachana na mambo ya mpira kwasasa anaishi Uturuki huko.

Alimaliza Paul Peter Kasunda.

Paul Peter Kasunda leo atakuwa uwanjani majira ya saa mbili [20:15] kuikabili Tabora United kwenye Dimba la CCM Jamhuri Jijini Dodoma.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine