Connect with us

Serie A

LEAO: SIPENDI MPIRA WA TAKWIMU KULIKO UBORA WA MCHEZAJI.

Nyota wa klabu ya AC Milan na timu ya Taifa ya Ureno, Rafael Leao ameweka wazi kuwa mpira wa sasa unaharibiwa kwa kiasi kikubwa na takwimu na hapendi namna mabavyo mfumo huo unatumika.

Leao anaamini kuwa mpira ni mchezo wa maajabu kuna siku ukiwa kwenye kiwango chako bora kabisa hakuna atakayekuja kukuzungumzia usipofunga lakini hata usipocheza vizuri ukafunga utazungumziwa sana.

Mpira wa leo ni wa takwimu zaidi, na sipendi hicho kitu, mpira wa miguu ni wa maajabu na furaha.

Inanifanya nichukie sana kuona watu wanafikiria zaidi namba, ukiwa na siku mbaya mchezoni lakini ukafunga watakusifia sana.

Amesema Leao.

Hadi hivi sasa ameitumikia AC Milan takribani michezo 196 na kufunga magoli 52 huku akitoa pasi za usaidizi wa magoli 44 akicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji wa kushoto.

Msimu huu ameendelea bora kwenye namba Rafael Leao, hadi hivi sasa amecheza michezo 33 kwenye mashindano yote, amefunga magoli 9 na pasi 8 za magoli, hivyo amehusika kwenye magoli 17 ya timu hiyo.

Makala Nyingine

More in Serie A