Connect with us

Makala Nyingine

ATLETICO MADRID YAPATA AHUENI UREJEO WA GRIEZMANN.

Atletico Madrid itashuka dimbani hii leo saa tano [23:00] kucheza mchezo wake wa pili wa Ligi ya mabingwa Barani Ulayà [UEFA] dhidi ya Inter Milan ikiwa nyumbani.

Atletico Madrid ilikubali kichapo cha goli 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora dhidi ya Inter Milan na leo inatazamia kupindua kibabe matokeo hayo na kufuzu hatua ya robo fainali.

Inter Milan ilicheza vyema kwenye eneo lake la ulinzi kwenye mchezo uliopita na kuifanya Atletico Madrid isipate shuti hata moja lililolenga lango.

“Naelewa kila kitu kinachoendelea kwetu, hadi kufikia mchezo wetu na Athletic Bilbao tulikuwa na msimu bora, ushindani lakini kwenye michezo michache timu haikuwa na ubora kama wa mwanzo, tutaendelea kukua zaidi kutokana na mafunzo tuliyoyapata.” – Diego Simeone.

“Mchezo wetu na Inter unahitaji umakini mkubwa, na lolote litakalotokea lazima tushinde.” – Diego Simeone.

Nyota wa klabu hiyo Antoine Griezmann aliumia Enka kwenye mchezo uliopita anatarajiwa kurejea kikosini kuelekea mchezo huu na kuwapa morali wana fainali hawa wa mwaka 2014 na 2016.

” Urejeo wake kwenye timu unatupa majibu mengi na uwezekano wa kutosha kiufundi na pia mchezo una muhitaji, wacha tuwe na matumaini atakuwa na mchezo anaotaka kucheza.” – Simeone.

Mlinzi wa klabu ya Atletico Madrid Axel Witsel amesema uwepo wa Griezmann unabadili aina ya uchezaji wa klabu hiyo.

“Grizzie anaipa nguvu sana timu, asipokuwepo ni tofauti kabisa, ni mchezaji mhimu sana kwetu na tunafurahi kuwa amerejea.” – Witsel alisema.

Kiungo Thomas Lemar na mshambuliaji Jose Gimenez ndio wachezaji pekee wa Atletico Madrid waliokosekana kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Inter Milan.

Inter Milan itawakosa mshambuliaji Marko Arnautovic ambaye atakaa nje ya uwanja kwa mwezi mzima na Carlos Augusto watakosekana kwenye mchezo wa leo.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine