Connect with us

CAF Champions League

MASHABIKI AL AHLY WAIHOFIA SIMBA ROBO FAINALI.

Mashabiki wa klabu ya Al Ahly baada ya kupangwa na klabu ya Simba kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika wameonyesha uoga kuelekea mchezo huo.

Baadhi ya mashabiki wanaona Simba ni klabu mgumu zaidi kwao kwenye hatua hii ya robo fainali, katika michezo mitano iliyopita Simba imeshinda [2] na imepoteza [1] na sare mbili [2].

“Ni timu ngumu, lakini sisi ni Al Ahly.” – Hossam Ahmed, Shabiki wa Al Ahly.

“Kila lakheri Al Ahly, hautakuwa mchezo rahisi, Mungu asaidie.” – Mohamed Eino, Shabiki Al Ahly.

Mashabiki wa Simba wameonyesha kufurahi zaidi kuliko ilivyo kwa mashabiki wa Al Ahly na wanaamini baada ya kuwa kizingiti kwa mida mrefu safari hii wanaweza kuwang’oa.

“Tulikuwa tunawataka nyie, na mjue tu kwa Mkapa hatoki mtu.” – Vanesa Puttin.

“Safari hii mtatusamehe, mechi hii tutaimaliza kwa mkapa.” – Job.

Simba imecheza mchezo jana na kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Singida Fountain Gate huku Al Ahly wakikipiga na National Bank wakachapwa 4-3.

Timu hizi zinatarajiwa kukutana kati ya March 29-30 na mchezo wa marejeano kati ya April 5-6 mwaka huu.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League