Connect with us

Makala Nyingine

MASHABIKI YANGA WAFANANISHWA NA KAIZER CHIEFS KUPIGA KELELE.

Baada ya klabu ya Mamelodi Sundowns kuchapisha taarifa ya mchezo wao wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya Yanga, mashabiki wengi wa Yanga walivamia page hiyo na kuandika sana.

Shabiki mmoja wa klabu ya Mamelodi Sundowns amewaweka kundi moja mashabiki wa Yanga na mashabiki wa klabu ya Kaizer Chiefs kwa kuwaita ni watu wenye kelele sana.

Shabiki hiyo ameeleza kuwa kelele ambazo Yanga wanazifanya kwasasa zitaisha baada ya mchezo wa kwanza kabla ya kwenda kuzimwa kabisa kwenye uwanja wa Loftus Versfeld.

“Inaonekana mashabiki wa Yanga na Kaizer Chiefs wana fanana, ni majirani wenye kelele, hawa watu wanapiga kelele sana.” – Mabongza Nkosi.

“Naamini watajutia maneno yao baada ya mechi ya kwanza, wanaweza wasisubirie mechi ya marejeano, kwasababu kile watakachokiona Loftus Versfeld ni majanga.” – Mabongza Nkosi.

“Wanaongea sana hawa jamaa, watakachokutana nacho watasimulia.” – Nthabisengi Sauidi.

Klabu ya Mamelodi Sundowns imecheza mchezo wa jana dhidi ya wapinzani wao wa karibu Supersport United unaitambulika kwa jina la Tshwane Derby ulioisha kwa sare ya 1-1, kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Loftus Versfeld.

Mchezo wa mwisho kwa Yanga wamecheza dhidi ya Ihefu na wakaibuka na ushindi wa goli 5-0 wakiwa nyumbani kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Michezo miwili ya klabu hizi mbili itapigwa kati ya March 29-30 na April 5-6 mwaka huu na Yanga itaanzia nyumbani na kwenda kumalizia ugenini nchini Afrika Kusini.

Mchezo huu unatazamiwa kuwa miongoni mwa michezo migumu zaidi kuwahi kuchezwa kwenye hatua ya robo fainali ikiwa inakutanisha timu Bingwa wa AFL [Mamelodi Sundowns] na Yanga iliyofika fainali ya kombe la shirikisho msimu uliopita.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine