Connect with us

Taifa Stars

SAKATA LA DICKSON JOB NA TFF LAIBUA WADAU WA SOKA.

Nyota wa klabu ya Yanga Dickson Job amekosekana kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kilichoitwa na kaimu kocha mkuu Hemed Suleiman jambo ambalo lilizua mijadala tofauti tofauti miongoni mwa wadau wa soka nchini.

Kwa mujibu wa taarifa zimaeleza kuwa nyota huyo [Dickson Job] aligoma kucheza eneo la ulinzi wa kulia kwenye mchezo dhidi ya Congo DR kwenye fainali za mataifa ya Afrika zilizokuwa zikifanyika nchini Ivory Coast.

Hata hivyo taarifa hiyo haijathibitishwa na mamlaka za soka nchini Tanzania, lakini baadhi ya wadau waliosafiri na timu hiyo walieleza jambo hilo huenda ndilo limesababisha Dickson Job asijumuishwe tena kwenye kikosi hicho.

Miongoni mwa wadau walioguswa moja kwa moja na tukio hilo ni Mtangazaji mkongwe wa Michezo nchini Alex Luambano na ametoa maoni yake juu ya sakata hili.

“Nimeona taarifa ya Dickson Job kukosekana kwenye kikosi cha Taifa Stars, nimefuatilia na kujua ni kwanini Dickson Job kakosekana, nimesikitishwa kuona kama Viongozi wa TFF wameshindwa kulimaliza hili bila drama za mitandao na vyombo vya habari.”

“Haya mambo yanatokea kwenye mpira na ilipaswa kuwa jambo la kumueka kijana chini na kukaa nae suluhu ipatikane, Msiingize vitu personal kwenye hatma ya mpira wa Nchi, Timu ya Taifa haiwezi kusajili mchezaji na Job ni mmoja kati ya mabeki bora nchini.” – Alex Luambano.

Timu iliyoitwa na kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman inaelekea kwenye michezo miwili ya kirafiki iliyoandaliwa na shirikisho la soka Duniani FIFA.

Makala Nyingine

More in Taifa Stars