Connect with us

NBC Premier League

SIMBA YABISHA HODI AZAM KUITAKA SAINI YA PRINCE DUBE.

Klabu ya Azam inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara imetoa taarifa kwa mashabiki na wadau ikieleza kuwa klabu za Simba na Al Hilal ya Sudan zimewasilisha ofa ya kuihitaji saini ya mshambuliaji wa klabu hiyo Prince Dube.

Kwenye taarifa waliyoitoa klabu hiyo inaeleza kuwa bado wanazitafakari ofa hizo huku wakiarika pia timu zingine kupeleka ofa mezani kwaajili ya kumnasa nyota huyo.

“Azam FC inathibitisha kwamba imepokea ofa kutoka vilabu viwili tofauti vikimhitaji mchezaji wwtu Prince Dube, raia wa Zimbabwe.”

“Ofa hizo zimetoka katika klabu za Simba ya Tanzania na Al Hilal ya Sudan.”

“Uongozi unazifanyia tathmini ofa hizo ili kuona ipi inafaa.”

“Aidha, Azam FC inazikaribisha klabu zingine kuleta ofa zao kwani milango bado iko wazi.”

  • Taarifa kutoka Azam FC.

Hata hivyo nyota huyo, Prince Dube amekuwa na msuguano wa kutaka kuvunja mkataba na klabu yake ya Azam na huenda kwa ofa hizi akaondoka rasmi Azam FC.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League