Connect with us

Makala Nyingine

KOCHA STARS: JOB ALIKOSA UZALENDO, KIMO CHAKE HAKIRUHUSU.

Mlinzi wa klabu ya Yanga Dickson Job hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania na kocha mkuu wa kikosi hicho Hemed Suleiman, jambo hilo liliibua hisia nzito kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Kaimu Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania [Taifa Stars] Hemed Suleiman ametolea ufafanuzi sababu za kutokumjumuisha kikosini nyota huyo licha ya ubora anaouonyesha kwenye klabu yake ya Yanga akitengeneza pacha na Ibrahim Hamad.

Kocha Hemed amesema sababu za Dickson Job kukosekana kwenye kikosi cha Taifa Stars ni kukosa uzalendo kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika zilizokuwa zinaendelea nchini Ivory Coast ambapo aligoma kucheza nafasi ya ulinzi wa kulia.

Kocha Hemed amewajia juu wale wote wanaomtetea Dickson Job na kuwaeleza kuwa hawamsaidii zaidi wanampoteza na kama yeye akiamua kulitolea ufafanuzi basi linaweza kumletea matatizo zaidi nyota huyo.

Kifupi ambao wanalizungumzia hili hawamsaidii Job, mimi na Job tumelizungumza yameisha salama, waheshimu maamuzi ya Mwalimu, watu wangeliacha kama lilivyo, mimi nikilitolea ufafanuzi nitamuua huyo.

Hemed Suleiman, Kaimu Kocha wa Taifa Stars.

Kwa mujibu wa kocha Hemed Suleiman ameeleza kuwa Dickson Job alikuwa anahitaji kucheza nafasi ya ulinzi wa kati lakini kwasababu ya kimo chake na falsafa za mwalimu Hemed hawezi kucheza nafasi hiyo.

Job anataka kucheza nafasi ya ulinzi wa kati lakini kwangu mimi na timu ya Taifa ni ngumu kwake yeye kulingana na kimo chake, anaweza kucheza nafasi hiyo lakini kwa mahitaji ya timu kwa sasa hawezi.

Kocha Hemed.

Kocha Hemed ameweka wazi kuwa Dickson Job baada ya mchezo wao dhidi ya Congo DR alimuomba msamaha na kumweleza kuwa kama ingetokea nafasi basi angaweza kucheza nafasi hiyo.

Mara ya mwisho wakati naongea nae baada ya mechi kumalizika [Congo DR 0-0 Tanzania] aliniambia anaweza kucheza kama kukitokea majeruhi yoyote, mimi nitachagua wachezaji kulingana na mechi ambayo tunacheza.

Aliendelea Kocha Hemed.

Kocha Hemed ameweka wazi kuwa Job bado ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na atamtumia pale ambapo atahitajika kutumika na atamtumia kwenye nafasi ya mlinzi wa kati kulingana na mahitaji ya mchezo husika.

Job bado ni mchezaji wa timu ya Taifa, nimekaa nae nimezungumza nae tumefikia mwafaka, badaae atarudi kwenye timu ya Taifa.

Kifupi tunahitaji wachezaji wa malengo ambao wanaweza kujitoa wakati wowote wanapohitajika kwenye timu.

Alimaliza kaimu kocha wa Stars.

Job kwasasa yupo kwenye kiwango bora sana akitengeneza pacha imara kwenye klabu yake ya Yanga na Ibrahim Hamad.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine