Connect with us

NBC Premier League

GAMODI AKIRI UGUMU KUCHEZA NA AZAM.

Kocha Gamondi amekiri kuwa wachezaji wake wanapitia kipindi kigumu sana hivi karibuni kutoka na uchovu wa mechi nyingi ndani ya muda mfupi.

“Licha ya ugumu wa ratiba bado tunayo njaa ya kupata alama tatu, hizi ni aina ya mechi ambazo unahitaji alama tatu kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda ubingwa.”

“Najua wachezaji wangu wanapitia nyakati ngumu kutokana na uchovu lakini nawahakikisha wanachi tutapigana mpaka tone la mwisho” .

“Kesho tutakuwa na mchezo mzuri sana kwa sababu timu zote mbili zinacheza soka safi, Azam FC wameonesha ukomavu wa hali ya juu msimu huu hivyo tuna kila sababu ya kujituma sana”

  • Miguel Gamondi
    Yanga kwasasa inaongoza Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ikiwa na alama 52 huku Azam fc ikiwa nafasi ya tatu ya msimamo na alama 44.

Mara nyingi Yanga na Azam zimekuwa zikitoa mchezo mzuri pindi zinapokutana licha ya kuwa asilimia kubwa ya michezo huwa ipo upande wa Yanga.

Hadi hivi sasa Yanga na Azam zimekutana mara 17 na mara hizo Azam imeshinda michezo minne [4] na Sare tano [5] huku Yanga ikishinda michezo nane [8].

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga iliibuka na ushindi wa goli 3-2 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League