Connect with us

Makala Nyingine

GAMONDI: NAJUA MAMELODI WAPO HAPA WANATUFUATILIA.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema leo kuwa anajua vitu vingi sana kuhusu Mamelodi Sundowns na ameanza kulifuatilia benchi la ufundi la klabu hiyo.

Gamondi ameweka wazi kuwa kwasasa bado hajaanza kuwafuatilia wachezaji wa Mamelodi Sundowns lakini kutokana na uzoefu alioupata miaka miwili ya utumishi pale unatosha kabisa kuisaidia timu yake.

Kocha huyo ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa hautakuwa mchezo rahisi lakini mwisho wa siku wachezaji 11 kila upande ndio watakaoamua mchezo wenyewe.

“Mamelodi Sundowns wapo hapa muda mrefu tu wanatutazama, lakini hatuna kitu cha kuficha, ndio tupo hivyo, mwisho wa siku wachezaji ndio wataamua uwanjani.”

“Siwezi kudanganya tumewatazama Sundowns, sio wachezaji bali benchi la ufundi, tumefanya kazi yetu lakini jicho letu lilikuwa ni dhidi ya Azam.”

“Nilikuja kwenye hii klabu kwasababu ilikuwa inashiriki Ligi ya mabingwa hiyo ilikuwa motisha kwangu lakini nimekuja hapa pia kushinda vikombe, hakuna kitu ambacho kitanitoa kwenye reli tunapamba kubeba ubingwa.”

“Sundowns ilikuwa sehemu ya maisha yangu, na nilibeba kombe langu la kwanza kama kocha kwenye taaluma yangu, na lilikuwa taji la kwanza kwa Patrice Motsepe wakati anainunua klabu.”

“Najua tamaduni zai, najua ari yao najua mambo mengi kuhusu wao kwa miaka miwili niliyokaa pale.” – Gamondi.

Yanga kwasasa inajiandaa na mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Jumapili katika dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

Baada ya mchezo huo wa kesho itabaki inajiandaa na mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa Jumamosi ya March 30 saa tatu [21:00] usiku.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine