Connect with us

NBC Premier League

MINGANGE: MZIZE ANGEKUWA PRISON ANGEFUNGA KILA SIKU.

Kocha Meja Mstaafu Abdul Mingange ameweka wazi kuwa kitu kinacho wafanya wachezaji wengi wa ndani ya Tanzania kuzidiwa uwezo na wachezaji wa kigeni ni kukosa misingi bora ya mpira tangu wakiwa vijana.

Mingange amewatolea mfano vijana wanaofanya bora kwasasa ambao amewafundisha na kuwapa misingi ya mpira tangu wakiwa vijana namna ambavyo wanapambana kama Lusajo Mwaikenda na Novatus Dismas Miroshi.

“Wachezaji wengi wa Tanzania wamekosa misingi, hasa kwenye technique na tactics, hapo ndio wanatushinda wachezaji wengi kutoka nje.”

“Wanakosa kwasababu academy nyingi hazina watu wenye uwezo, Lusajo alikuja kwenye academy ya Azam akakaa miezi miwili anakuja na kuondoka, hakuna kunywa chai wala kulala, mpaka nilipomuona sasa huyu anaweza kuingia ndio nikamuingiza.”

“Nimekaa nae miaka miwili, yule na Novatus Dismas ambaye alikuja anacheza beki ya kushoto lakini kwasababu ya urefu wake nikamchezesha namba sita.” – Meja Mstaafu Abdul Mingange.

Kwa upande mwingine pia Kocha Meja Mstaafu Mingange ameweka wazi kuwa kwenye timu zote za Tanzania kwenye madaraja yote hakuna mshambuliaji hatari kama Clement Mzize lakini kilichokosekana kwake ni misingi ya soka.

Mingange ameeleza kuwa nyota huyo hata hivyo anapambana zaidi jambo ambalo limemfanya ahusike kwenye ufungaji magoli ya timu yake Yanga kwenye michezo mikubwa na ya kimataifa.

Mingange anaeleza kuwa kuna wakati anashindwa kuwa bora kutokana na ukubwa wa timu anayoitumikia lakini angekuwa timu kama Prison basi angekuwa anafunga kila siku.

“Mzize ni Nabi, watu wengi wana mlaumu lakini wanakosea sana kwasababu anakuwa bora kila siku zinavyoenda.”

“Watu wanataka kumkatisha tamaa, wanataka afanye vitu vikubwaa, yule hana msingi wa mpira, hata hivyo anajitahidi sana anaenda vizuri, anapiga miguu yote, ana nguvu, ana mbio anapiga kichwa vizuri.”

“Yule mtu atakuwa mshambuliaji mzuri sana lakini sisi tunataka vitu vya uharaka, yule kakosa msingi lakini angepita kwenye njia nzuri wala hayupo hapa Tanzania.”

“Ukiangalia kwenye timu zote za Taifa katika mchezaji anayeweza kukupa kitu yule anakupa kitu, yule anatakiwa aaminiwe, sasa anacheza timu kubwa, ambayo wanataka matokeo kila wakati.”

“Angekuwa timu kama Prison, Dodoma Jiji yule kila mechi angekuwa anafunga.” – Meja mstaafu Abdul Mingange.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League