Connect with us

Bundesliga

HALLER: NILIPO IKOSESHA UBINGWA TIMU ILIUMA KULIKO CANCER.

“Nilikuwa natembea kushuka ngazi za uwanja, nilisikia watu wananizomea wakisema ‘wewe haunafaida, kucheza hauchezi, unafanya matangazo tu’, nilijihisi nimekufa ndani yangu.”

Hayo ni maneno ya mshambuliaji nyota wa klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki Ligi kuu nchini Ujerumani na na timu ya Taifa ya Ivory Coast.

Aliyazungumza hayo baada ya Ivory Coast kupoteza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi ya AFCON 2023 dhidi ya Equatorial Guinea walipokubali kichapo cha goli 4-0, kwenye dimba la Alassane Ouattara.

Sebastien Haller hakupata nafasi ya kucheza kwenye michezo ya mwanzo ya hatua ya makundi kutokana na majeraha ya Enka lakini bado alizomewa na mashabiki.

Ikumbukwe Ivory Coast walikuwa wenyeji wa michuano hiyo, iliwalazimu kusubiri hadi michezo mingine ya hatua ya makundi imalizike ili kuona kama watafuzu hatua inayofuata huku wakiiombea mabaya Zambia mbele ya Morocco na mwisho wakafuzu kama bestloosers.

Wiki tatu baadae uwanja ule ule wa Alassane Ouattara, Sebastien Haller akafunga goli la ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya timu ya Taifa ya Nigeria.

Kwa Haller jambo hilo lilikuwa kama zawadi kwa kila kitu ambacho aliwahi kukipitia tangu alipolazwa kwa tatizo la Cancer kwa miezi 18 iliyopita.

Haller alijiunga na kikosi cha Borrusia Dortmund akitokea Ajax kwa ada ya €34.5 Million akiziba nafasi ya Erling Haaland aliyetimkia Manchester City lakini wiki kadhaa nyuma wakati klabu hiyo ya Borussia Dortmund ikiwa inajiandaa na msimu mpya Haller alianza kulalamika kuwa anapata maumivu kuzunguka tumbo lake.

Haller alijaribu kuwasiliana na daktari wake na walifanya vipimo kadhaa lakini hawakufanikiwa kutibu tatizo, baada ya hapo akawatafuta madaktari wa timu na kisha kumfanyia vipimo ambapo waligundua kuna kitu kinasababisha maumivu tumboni.

Haller anasema ” Nilipokuwa Dortmund, niliwaomba madaktari kama ingewezekana wanifanyie uchunguzi na wakaona kitu ambacho kilikuwa kinasababisha maumivu.”

“Nilifanya MRI scan na siku iliyofuata waligundua kuna uvimbe, walihitaji kuangalia kama ilikuwa mbaya au ilikuwa bado, tuliangalia baada ya mazoezi na ndani ya dakika 30, madaktari waliniambia “Unahitaji kufanyiwa upasuaji na tunapaswa kufanyiwa leo au kesho.”

Haller alikubaliana na swala la upasuaji lakini alihitaji kujua ni nini hasa kinachomsumbua lakini alikuja kujua ni Cancer “Niliwauliza ni nini hasa ?, na baadae nilijua ni Cancer, haya ni maneno magumu na yanaogopesha kwa kila mtu, hakuna anayetamani kuwa nayo, lakini ukipata Cancer, utaielewa zaidi.”

Haller alipitia upasuaji ili kuuondoa uvimbe ule kisha akaanza matumizi ya dawa kali jambo ambalo lilimfanya alale hospital kwa siku tano akitumia mirija.

Alipitia hatua za tatu za matibabu na hatua ya pili ya upasuaji ulikuwa wa kuondoa mabaki yaliyobaki kwenye uvimbe uliokuwa umepatikana.

Kwa wakati wote huo Haller alikuwa akipata ushirikiano wa karibu kutoka kwa mke wake Priscilla na watoto wake watatu pamoja na ndugu zake Armelle na Sery.

Wakati anaendelea kujiuguza alikuwa akitumia muda wake mwingi kutembelea Cannes na marafiki zake ambapo alikuwa anaenda kucheza golf.

October 2022 alikuwa sehemu ya watu waliohudhuria sherehe za utoaji tuzo za Ballon D’or zilizofanyika Paris, Ufaransa na alipigiwa makofi mengi sana alipoitwa kutoa tuzo.

Haller alipoulizwa kuhusu kustaafu kucheza soka alikiri kuwa hana huo mpango lakini amekutana na changamoto tu ambazo zikiisha atarudi tena uwanjani, hakukata tamaa.

Haller anasema “Unakuwa mtu mwingine lakini hauwezi kutambua, unajaribu kufanya kila uwezalo lakini bado utateseka, watu wa karibu yako watajaribu kuficha huzuni na hisia zao lakini ni ngumu.”

“Unakuwa na uvumilivu kidogo, hasira na unakuwa mwenye hisia kali, wakati ambao kila mmoja anajaribu kuficha hisia zao na kubadili mitazamo inakuwa ni ngumu sana, mawasiliano ni kila kitu.”

December 2022, Haller aliruhusiwa kurudi tena uwanjani na kuanza kucheza tena baada ya kupona . Alijiunga na kikosi cha Dortmund kilichokuwa kwenye maandalizi ya msimu huko Marbella na alifunga goli 3 ndani ya dakika saba kwenye ushindi wa goli 6-0 wa Dortmund dhidi ya Basel ya Uswiss.

Haller alicheza mchezo wake wa kwanza wa ushindani baada ya kurejea dhidi ya Augsburg wakati Dortmund ikishinda 4-3.

February 4, ambayo ni a
Siku ya Cancer Duniani alifunga goli lake la kwanza baada ya kurejea uwanjani dhidi ya Freiburg.

Haller anasema “Kila mmoja anaweza kuumwa lakini unapaswa kusimama pale utakapoanguka, utapata usaidizi kutoka kwa familia na marafiki zako na ufurahie kila muda utakaopata.”

Mwishoni mwa msimu wa 2022-23 Haller alifunga magoli 8 kwenye mechi 10 na kidogo aipatie ubingwa wa Bundesliga klabu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10.

Borussia walikosa ubingwa baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Mainz siku ya mwisho na Haller alikosa penalty na Jamal Musiala akaifungua goli la ushindi Bayern dakika za mwisho dhidi ya Cologne na Bayern kutwaa ubingwa kwa tofauti ya magoli.

“Ilikuwa ni huzuni kubwa niliyowahi kuipata kwenye mpira wa miguu, ilikuwa ngumu kuikubali kuliko ugonjwa wangu, kwasababu ningekuwa na faida juu ya hilo, ilikuwa sio janga tu zaidi ya maigizo, niliumia sana.”

“Kwenye wakati kama huu, unagundua kuwa una bahati na umebarikiwa kuwa na familia na marafiki wanaokuzunguka, kama ningekuwa mwenyewe, pengine ningebaki nimekaa uwanjani kwa wiki moja bila kutikisika.”

Mama yake Sebastien Haller alizaliwa na kulelewa kwenye mji wa Gagnoa ambao upo takribani Mile 145 kutoka Jiji la kiuchumi la Ivory Coast la Abidjan na akahamia Ufaransa alipokuwa na miaka 18 alipokutana na Haller [Baba yake Sebastien].

Haller alizaliwa karibu na Jiji la Paris na aliiwakilisha Ufaransa kwenye timu za umri tofauti tofauti ikiwemo chini ya miaka 17 kwenye fainali za kombe la Dunia 2011 ambapo alicheza pamoja na Aymeric Laporte na Kurt Zouma.

Baadae alibadili Taifa na kuhamia Ivory Coast ambapo rasmi November 2020 aliitumikia kwa mara ya kwanza timu ya Taifa ya Ivory Coast kwenye mchezo dhidi ya Madagascar wakiibuka na ushindi wa 2-1.

“Nilipokuwa Westham, nikuwa naongea na kocha wa Ivory Coast, Patrice Beaumelle ambaye alikuwa anataka sana niitumikie Ivory Coast, kama Baba nilihitaji kuwa karibu na taifa langu la asili.”

Kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga kabla ya mapumziko ya kipindi cha Baridi Haller aliumia Enka wakati ambao AFCON inakaribia, na madaktari wa Dortmund wakampa miezi mitatu ya kupumzika.

Lakini kocha wa Ivory Coast Jean Louis Gasset alimjumuisha kikosini nyota huyo pamoja na nyota wa Brighton Simon Adingra aliyekuwa majeruhi kwenye kikosi.

Nyota hao waliwekwa kwenye uangalizi maalumu wa madaktari wakiwa na matumaini kuwa watarejea kwenye michezo ya mtoano.

“Nilitumia muda mwingi kwenye mashindano kwenda kunywa chai, kupata matibabu, kwenda Gym, matibabu Gym, nilikuwa namaliza saa saba usiku kwasababu nilikuwa nafanya kazi zote hizl”.

Ivory Coast walishinda mechi ya kwanza ya ufunguzi, wakapoteza mbele ya Nigeria na dhidi ya Equatorial Guinea na kuiacha nafasi yao ya kusonga mbele kwenye hatihati kubwa.

Haller anasema “Ilikuwa kama ndoto, unahisi hakuna kitu kinachofanyika kama unavyotaka, umekuja, uko majeruhi, huwezi kucheza na unaondolewa kwenye mashindano, ilikuwa ni upotevu wa nguvu na muda wa watu wengi na pesa kwa wengine pia, ilikuwa ni ndoto ambayo ilikuwa inatoweka.”

Ushindi wa morocco wa 1-0 dhidi ya Zambia uliwasaidia Ivory Coast kufuzu hatua iliyofuata kama bestlooser kwenye nafasi ya tatu na walikuwa wanaenda kukutana na mabingwa wa AFCON 2021 timu ya Taifa ya Senegali.

Shirikisho la soka nchini Ivory Coast likamtimua kazi kocha wake Gasset na nafasi yake ikachukuliwa na msaidizi wake Emerse Fae, japo Ivory Coast ilijaribu kumuajiri kocha wao wa zamani Herve Ranard ambaye kwasasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa ya wanawake lakini ilishindikana.

Ivory Coast waliiondosha Senegal kwa mikwaju ya Penalty, wakaifunga Mali nusu fainali 2-1 na kukutana na Nigeria ambayo ilikuwa na safu bora ya Ulinzi kwenye mashindano lakini Haller alifunga goli la ushindi kwa timu yake na kuipa ubingwa.

Kocha wa muda wa Ivory Coast Emerse Fae alisema ilikiwa zaidi ya kuzimu.

Haller akasema “Hata sijui iliwezekana vipi, lilikuwa letu tu, tunaweza kuelezea lakini ukweli ni kuwa hatuendeshi chochote.”

Makala Nyingine

More in Bundesliga