Connect with us

Top Story

ROBINHO KUFUNGWA JELA MIAKA 9 KISA UNYANYASAJI WA MWANAMKE.

Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester City na timu ya Taifa ya Brazil Robinho anatarajiwa kutumikia kifungo chake cha miaka tisa [9] jela huko nchini kwao Brazil.

January 22, 2013: Nyota huyo na wenzake tisa [9] walikutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono kwa mwanamke raia wa Albania wakati akiwa anaitumikia klabu ya AC Milan.

2014: Vyombo vya habari nchini Brazil viliripoti kuhusu hilo jambo lakini mambo yaliendelea kutokuwekwa wazi kwa kipindi hicho.

2017: Robinho alikutwa na hatia na mahakama ya nchini Italia na akahukumiwa kwenda jela miaka tisa [9], alikana makosa hayo na kukata rufaa.

2020; Baada ya rufaa yake, kifungo cha miaka tisa [9] kiliendelea kusalia na alitakiwa aende jela lakini kutokana na sheria za Italia hakuruhusiwa kufungwa nchini humo.

2023: Robinho alipeleka passport zake zote kwenye mamlaka ya nchini Italia.

November 2023: Askari wa nchini Italia wakasema wamemuachia Robinho hivyo ataenda kutumikia kifungo hicho nchini kwao Brazil.

March 20, 2024: Mahakama ya juu ya nchini Brazil ilitengeneza kamati ndogo na wakapiga kura kuhusu Robinho kuitumikia adhabu hiyo nchini kwao.

Makala Nyingine

More in Top Story