Connect with us

NBC Premier League

TAHARUKI TABORA UNITED

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani Tabora zinadai kuwa kocha mpya wa Tabora United Denis Laurence huenda akatimka kikosini hapo baada ya siku chache tangu alipojiunga na kikosi hicho akichukua nafasi ya Goran Kopnovic.

Sababu za kocha Denis kutimka zinadaiwa kuwa amekutana na mazingira tofauti na yale aliyoambiwa na aliamini Tabora inafanana na Dar Es Salaam.

Licha ya kuanza kusimamia mazoezi ya klabu hiyo lakini yeye na kocha wake msaidizi Masoud Djuma bado hawajasaini mkataba na klabu hiyo.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa huenda kocha msaidizi Masoud Djuma akakabidhiwa na kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ya Tabora United.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League