Connect with us

Boxing

DULLAH ALIMJUA VIZURI MPINZANI WAKE?

Usiku wa tarehe 31/03/2024, Bondia kutoka Nchini Tanzania Abdallah Pazi maarufu Dullah Mbabe alipoteza pambano la Uzito wa Kati dhidi ya Bondia kutoka Barnsley, Uingereza Callum Simpson.

Dullah alipoteza pambano hilo la Raundi 10 katika raundi ya 4 kwa KO baada ya kudondoshwa na bondia huyo aliyekuwa akitetea mkanda wake wa WBA- Super Middleweight kwenye Usiku ambao Pambano Kuu lilikuwa kati ya Fabio Wardley na Frazer Clarke lililomalizika kwa Sare pale O2 Arena.

Watanzania wengi wakaja na maswali juu ya maandalizi kutoka kwenye kambi ya Dullah kuelekea pambano hilo huku wengine wakihoji kama alijua anakwenda kupambana na bondia wa kaliba gani.

Callum Simpson kabla ya pambano lake na Dullah alikuwa amekwishapigana mapambano 13 huku akishinda yote 13, 8 yakiwa kwa KO/TKO kwenye Uzito huo wa Kg 76-78 huku pambano lake la mwisho alipigana na Jose De Jesus Maceas na kushinda kwa Unanimous Decision tarehe 30/09/2023.

Mwezi Februari 2023, Wakati anatangaza kuwa atapigana tarehe 31/03/2024 bado haikujulikana anapigana na nani huku Dullah akija kupost kwenye Ukurasa wake Wiki 2 kabla ya Pambano.

Makala Nyingine

More in Boxing