Connect with us

Makala Nyingine

TFF NA CRDB MAMBO SAFI FA

Shirikisho la soka la Tanzania, TFF na Benki ya CRDB leo wameingia makubaliano ya Udhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho(FA).

TFF kupitia Rais wake Wallace Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndugu Abdulmajid Nsekela walisaini mkataba wa Miaka mitatu(3) wenye thamani wa zaidi ya Bilioni 3 na sasa Kombe hilo litatambulika kama CRDB Bank Federation Cup.

Itakumbukwa Mkataba wa Mwisho uliohusisha TFF na Mdhamini wa Kombe la Shirikisho ni ule wa Azam Media(ASFC) wa miaka 4 uliosainiwa Septemba, 2019 wenye thamani ya Bilioni 4.5.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine