Connect with us

Ligi Nyingine

NDONDO CUP 2024: IELEWE MITAA, USAJILI TIMU WAFUNGULIWA

Usajili wa Timu kwa ajili ya Mashindano maarufu ya Ndondo Cup mwaka huu 2024 yakiwa yamebeba Kauli ya IELEWE MITAA umefunguliwa rasmi na sasa timu zinaweza kuanza kwenda kusajili timu zao kwa ajili ya msimu huu.

Fomu za Usajili za Ndondo Cup 2024: Ielewe Mitaa zinapatikana kwenye ofisi ya DRFA zilizopo Ilala kwa shilingi Laki 3 tu(300,000/=) huku mchakato wa Zawadi mbalimbali ikiwemo kifuta jasho pia ukiwekwa wazi.

Itakumbukwa kuwa Bingwa mtetezi wa Ndondo Cup ni timu ya Madenge ambayo imechukua kwa mara ya 2 mfulululizo, Msimu wa 2022 na 2023.

Ndondo Cup 2024 imebeba dhana hiyo ya IELEWE MITAA ikimaanisha kuwa ni zaidi tu ya Mashindano ya Soka bali licha pia ya Kutoa Fursa kwa Wanasoka kuonyesha vipaji vyao na kutimiza ndoto zao, Wajasiriamali kufanya biashara zao lakini pia ni wakati wa watu kutambua Mitaa yao na Viongozi wao wa maeneo wanayoishi.

ufafanuzi huu ulitolea na Muasisi wa mashindano haya, Ndugu Shaffih Dauda.

Huu ni msimu wa 11 wa Ndondo Cup tangu kuasisiwa kwake huku msimu wa 10 ulibeba Kauli ya FAMIASALA NINI?!

Makala Nyingine

More in Ligi Nyingine