Azam FC

AZAM FC KUMKOSA BANGALA JUMATATU.

Ofisa habari wa klabu ya Azam Hashim Ibwe amesema timu yake ipo tayari kupambana na Yanga Jumatatu.

Published on

Kuelekea katika mchezo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara kati ya Young Africans dhidi ya wana lambalamba klabu ya Azam FC, Ofisa habari na mawasiliano wa klabu ya Azam Hashim Ibwe amesema kuna uwezekano wa kumkosa nyota wao Yannick Bangala katika mchezo huo kutokana na majeraha madogo aliyoyapata licha ya kuanza mazoezi chini ya uangalizi wa Daktari wa klabu hiyo.

Wachezaji wengine ambao wanaweza kukosekana kwa upande wa Azam katika mchezo huo ni Yahya Zayd ambaye ana majeraha madogo na tayari ameanza mazoezi chini ya uangalizi wa daktari wa viungo, na Abdallahkheri Sebo ambaye alifanyiwa upasuaji wa goti.

Mchezaji ambaye amethibitishwa kuukosa mchezo huo ni Abdallah Sebo ambaye ana majeraha ya goti na alienda kufanyiwa upasuaji kule Afrika Kusini, tulitoa taarifa hiyo mapema bado ana miezi miwili takribani na wiki moja ya kuendelea kujiuguza, lakini Yahya Zayd na Yannick Bangala wao walipata majeraha madogo madogo wanaendelea kufanya mazoezi ya viungo na Physician wetu, pale ambapo itaamuliwa kwamba wapo tayari kwaajili ya huo mchezo watacheza

Hashim Ibwe Ofisa habari wa Klabu ya Azam.

Kwa upande mwingine Azam FC ipo tayari kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Young Africans, mchezo huo utapigwa Jumatatu, October 23, katika Dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

https://daudasports.co.tz/wp-content/uploads/2023/10/Hashim-Ibwe-.mp3
Ofisa Habari wa Azam fc akieleza maandalizi ya timu yake na hali ilivyo kuelekea mchezo dhidi ya Young Africans Jumatatu October 23.

Popular Posts

Exit mobile version