17:00 SIMBA vs YANGA
UWANJA: BENJAMIN MKAPA
Kuelekea katika mchezo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara unaowahusisha watani wa jadi klabu ya Simba mwenyeji wa mchezo na klabu ya Yanga, katika Jiji la Dar Es Salaam leo mvua imenyesha kuanzia asubuhi hali ambayo inawafanya baadhi ya mashabiki kuwa na hatihati ya mchezo huu kufanyika.
Dauda sports ilipata nafasi ya kuzungumza na Afisa habari wa bodi ya Ligi Tanzania Karim Boimanda ambaye amewatoa hofu mashabiki wa soka nchini na kusema kuwa mchezo uko palepale na hakuna kitakachobadili hadi wakati wa mchezo utakapofika.
Mchezo uko pale pale na hakuna kitakachokwamisha, huu ni uwanja bora mpira utachezwa na watu tayari wameanza kuingia uwanjani.
Karim Boimanda, Afisa habari wa bodi ya Ligi akizungumza na Daudasports.