Kocha wa zamani wa Mbeya City miongoni mwa timu zingine, Abdallah Mubiru, ametambulishwa rasmi leo kama Kocha Mkuu wa klabu ya soka ya KCCA ya Uganda kwa mkataba miaka miwili akichukua nafasi ya kocha Mreno Sergio Daniel Traguil, walieachana nae Oktoba mwaka huu.
Mubiru anakuwa kocha wa KCCA kwa mara ya pili kwenye maisha yake ya ufundishaji, baada ya kuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2014. Uzoefu wake na klabu hiyo haipo tu kwenye ufundishaji bali pia aliwahi kuichezea kwenye miaka ya 90 hivyo anaifahamu hasa na zaidi falsafa za timu.
Jukumu kuu la kwanza la mwalimu Mubiru na benchi lake la ufundi ni kuirudisha KCCA kwenye njia sahihi ya msimu huu bada ya kuonekana wamepotea huku wakipata ushindi wao wa kwanza msimu huu dhidi ya Vipers kwa kuwanyuka 3-1 baad ay kucheza zaidi ya mechi 5 bila ushindi.
Abdallah Mubiru ameaminika na uongozi wa KCCA kutokana na uzoefu wake wa soka la Ugangda pia kwani amewahi kuwa kocha wa Polisi FC, Vipers SC na timu ya taifa ya Uganda, Uganda Cranes pia.