Timu za Taifa za Wanawake za Tanzania

TWIGA STARS KUIWINDA AFRIKA KUSINI FEB. 11.

Published on

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania [Twiga Stars] Bakari Shime leo ameita kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini kuikabili timu ya Taifa ya Afrika Kusini.

Twiga Stars itaingia kambini February 11, kwaajili ya kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu michuano ya Olympic.

Hata hivyo kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania [Twiga Stars] hajamjumuisha kikosini nyota wa zamani wa klabu ya Yanga Aisha Masaka kutokana na majeraha aliyonayo.

Nyota waliounda kikosi cha wachezaji 24 watakaoingia kambini February 11 ni;

GOLIKIPA.

  • Najat Abbas – JKT Queens
  • Asha Mrisho – Aman Queens
  • Husna Mtunda – Yanga

WALINZI.

  • Julieth Singano – Juarez [Mexico].
  • Anastazia Katunzi – JKT Queens
  • Christer Bahera – JKT Queens
  • Fatma Issa – Simba Queens
  • Violeth Nicholaus – Simba Queens
  • Happy Hezron – JKT Queens.

VIUNGO

  • Esther Mabanza – JKT Queens
  • Aquila Gasper – Fountain Princess
  • Stumai Abdallah – JKT Queens
  • Enekia Kasonga – Estern Flames [Saudi Arabia].
  • Joyce Lema – JKT Queens
  • Janeth Christopher – JKT Queens
  • Amina Bilal – JKT Queens
  • Diana Lucas – Ame S.F.K [Uturuki].
  • Hasnat Ubamba – Fountain Gate Princess.
  • Irine Kisisa – Yanga Princess

WASHAMBULIAJI

  • Opa Clement – Besiktas [Uturuki]
  • Aisha Juma – Simba Queens
  • Donisia Minja – JKT Queens
  • Winfrida Gerald – JKT Queens
  • Jamila Rajab – JKT Queens.

Kikosi cha Twiga stars kimeundwa na wachezaji 12 kutoka klabu ya JKT Queens, Mmoja [1] Aman Queens na wawili [2] Fountain Gate Princess inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara kwa upande wa wake.

Nyota wengine wanne [4] wametoka kwenye klabu za nje ya nchi.

Popular Posts

Exit mobile version