Top Story

FRANK: URENO WAKIENDA NA RONALDO HAWABEBI EURO.

Published on

Nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ufaransa Frank Leboeuf anaamini kuwa Ureno haitaweza kuchukua Euro 2024 ikiwa na Cristiano Ronaldo.

Leboeuf anasema kama Ureno haitamjumuisha Ronaldo kwenye kikosi chao basi dhahiri wanaweza kuwa washindani wa kombe la Ulaya [Euro 2024].

Kwangu mimi, Ureno ni miongoni mwa timu zitakazokuwa kwenye nafasi ya ubingwa wa Euro 2024 majira haya ya joto.

Nafikiri wanaweza kuwa mabingwa wa Euro, lakini kama tu Cristiano Ronaldo hatacheza.

Frank Lebouef.

Ronaldo anaamini bado ana nguvu ya kuisaidia timu yake ya Taifa ya Ureno na ana mategemeo makubwa kuwa atakuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachokuwa kikisaka kombe la pili la Euro.

Popular Posts

Exit mobile version