NBC Premier League

NYOTA WA ZAMANI SIMBA AWEKA UBORA WA CHAMA NA PACOME.

Published on

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Mtemi Ramadhan leo akizungumza na kitu cha habari cha EFM amewaeleza nyota wawili walio kwenye kiwango bora sana kwasasa nchini Clatous Chama [Simba] na Pacome Zouzoua [Yanga].

Mtemi ameeleza kuwa nyota Clatous Chama na Pacome Zouzoua wanatofauti nyingi kati yao lakini licha ya hivyo bado kila mmoja anakitu cha ziada huwezi kumfananisha na mchezaji mwingine.

Mtemi amesema kuwa Chama anaujua sana mpira kuliko Pacome lakini Chama anazidiwa utimamu wa mwili na Pacome Zouzoua na laiti kama nyota huyo angekuwa na utimamu wa mwili basi angeisaidia Simba kubeba Ubingwa wa Afrika.

Chama anaujua sana mpira kuliko Pacome lakini anazidiwa utimamu wa mwili na Pacome, kama ingekuwa ni kununuliwa Ulaya Pacome angeenda na Chama akabaki.

Laiti kama Chama akiwa na utimamu wa mwili kama alivyo Pacome, kwasasa hivi tunavyoongea Simba ingekuwa imebeba kombe la Afrika.

Mtemi Ramadhani, Kiungo wa zamani wa klabu ya Simba.

Kwasasa klabu zao zote mbili za Simba na Yanga zimefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika na droo itachezeshwa March 12, 2024.

Pacome huu unakuwa msimu wake wa kwanza kuwa na klabu ya Yanga huku Chama akiwa na Simba kwa zaidi ya misimu minne sasa tangu aliposajiliwa licha ya kuondoka kwenda Berkane na kisha kurejea tena.

Popular Posts

Exit mobile version