Makala Nyingine

SIMBA YAZINDUA KAMPENI KUELEKEA AFL

Published on

Klabu ya soka ya Simba leo imezindua rasmi kampeni zake kuelekea mchezo wao wa ufunguzi wa African Football League dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa Ijumaa ya Tarehe 20/10/2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

CEO wa Simba Ndg. Imani Kajula alitoa shukrani zake wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Serena.

Tunaishukuru serikali kwa matengezo makubwa ambayo imefanya kwenye Uwanja wa Mkapa. Simba pia imetoa mchango kiasi kufanikisha hili.

Rais wa FIFA atakuwepo, Rais wa CAF atakuwepo na marais wa vyama vya soka vya maeneo mengine hivyo inahusisha vyombo vingi za serikali.

Katika upande mwingine, Kajula hakuacha kuwasihi mashabiki kufika kwa wingi kwenye mchezo huo huku pia akielezea mchakato wanaofanya kurahisishia mashabiki kufika uwanjani bila usumbufu ikiwemo unafuu wa safari za anga.

Tunajua kutakuwa na watu mbalimbali kutoka mikoani na jana tulikuwa na mkutano na Air Tanzania ili kupata punguzo la bei ya tiketi kwa mashabiki wa Simba kutoka mikoani.

Lengo letu ni uwanja kujaa watu 60,000. Tunatarajia tiketi zitauzwa kwa haraka hivyo tiketi zikitangazwa watu wanunue kwa haraka sababu tunatarajia watu wengi kutoka nje ya Dar. Tiketi za makundi zitaendelea kuwepo (Mnyama Package).

Wakati huo huo Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally naye aliwatangazia mashabiki uzinduzi wa wiki ya hamasa(wiki ya kispika) kuwa itakuwa tarehe 14/10/2023 siku ya Jumamosi na kuendelea mpaka siku ya mchezo wenyewe akiwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Tutazunguka Dar nzima kufanya hamasa. Tarehe 14 ndio tutazindua wiki ya Kispika (Wiki ya Hamasa), tutazindulia Coco Beach. Kutakuwa na matukio mbalimbali kama mechi za mashabiki na pia kutakuwa na watu wa kuuza tiketi, watu wa NMB na CRDB kwa ajili ya watu kupata namba za mashabiki lakini pia jezi zitauzwa pale.

Hii ni wiki yetu, kama kuna mtu kinamkera aende hata Tanga. Hiyo tarehe 14 tutaanzia maandamano kutokea makao makuu ya klabu kwenda Coco Beach. Tunatarajia kufika Coco majira ya saa 4 asubuhi.

Jumapili itakuwa mapumziko kidogo. Jumatatu tutakuwa na Paint the City, hiyo siku ni kubandika vipeperushi kila sehemu. Kwenye mstimu, kwenye geti, kwenye magari. Hakuna mtu ambaye hatajua kama Simba inacheza tarehe 20.- Ahmed Ally. 

Katika hatua nyingine Ahmed Ally alitangaza gharama za tiketi na kwamba tayari zimeshaanza kuuzwa kwenye vituo vyote vya kuuzia tiketi huku akisema kuwa hakutakuwa na tiketi za VIP A kwakuwa jukwaa limeshachukuliwa na CAF na FIFA.

Viingilio tumepanga kwa kuangalia hali za watu wetu.
Platinum – Tsh. 200,000
VIP B- Tsh. 40,000
VIP C – Tsh. 30,000
Machungwa – Tsh. 10,000
Mzunguko – Tsh. 7,000.

Popular Posts

Exit mobile version